Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

eeee

ad1

4x4

bendela

.

Tuesday, December 1, 2015

HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

SIMU.TV: Mwili wa aliyekuwa mfanyakazi wa Azam Media Ismail Hamza unatarajiwa kusafirishwa kesho na kuzikwa mkoani Morogoro.https://youtu.be/fQx7_HOcHVM

SIMU.TV: Jumla ya walemavu 65 nchini wamepatiwa msaada wa miguu mbadala na kampuni ya Kamal Steels kwa lengo la kuwasaidia kutembea.  https://youtu.be/aYgsa2IAGLU

SIMU.TV: Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amewataka wakazi wa Mkoa huo kujiunga na kituo cha kuwezesha wananchi kujikwamua kiuchumi POSO ili kupata mitaji ya kujiendeleza kiuchumi;https://youtu.be/9eiTOAdDYf8

SIMU.TV: Wananwake Mkoani Mbeya walalamikia waume zao juu ya matumizi nabovu ya  fedha za TASAF wanazopokea kutoka serikalini; https://youtu.be/wzoJsMdzQSA

SIMU.TV:  Rais Magufuli ametoa agizo kwa wenyeviti na wakurugenzi kusimamia mashirika ya umma na hukakikisha yanazalisha ili kuingizia taifa faida;https://youtu.be/_elnHPUbHyI

SIMU.TV: Hali ya taharuki imeibuka katika mtaa wa Nyasaka B Mkoani Mwanza baada ya mkazi mmoja kumfungia mtoto wa miaka 2 ndani ya nyumba;https://youtu.be/OVGF2FVs-Jc

SIMU.TV: Serikali yawataka wananchi wote kushiriki katika zoezi la usafi siku ya Uhuru kama kutii agizo la Rais Magufulihttps://youtu.be/mf611qpGt40

SIMU.TV: Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ametoa siku 3 kwa viongozi wa manispaa za mji huo kuhakikisha wanaondoa taka katika maeneo yao ili kuepukana na mlipuko wa kipindupindu https://youtu.be/BgJzjfICyI4
SIMU.TV: Timu ya soka ya Tanzania chini ya miaka 15 inatarajia kuanza ziara yake ya mafunzo kwa nchi za Afrika Mashariki kwajili ya kujiandaa na michuano ya kimataifa; https://youtu.be/rwZQUGdICoo

TBC: Tanzania imeendelea kupata changamoto uanzishwaji wa ligi ya mpira wa miguu kwa wanawake jambo linalopelekea changamoto kwa wadau wa soka nchini; https://youtu.be/29UzpEUNTWQ

Regards

CCM YAAHIDI KUMPA.USHIRIKIANO DK. MAGUFULI:

             
     Rais, Dk John Magufuli akiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

 NA BASHIR NKOROMO
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema, kitampa ushirikiano mkubwa, Rais Dk. John Magufuli, ili aweze kwa ufanisi zaidi mapambano yake dhidi ya mafisadi na mikakati mingine ya kuinua uchumi wa Watanzania.
Kimesema, kitampa ushirikiano huo Rais Dk. Magufuli, kwa sababu, aliyoanza kuyafanya na atakayoyafanya baadaye katika uongozi wake wa Urais anatekeleza yale yaliyomo katika ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020.
Hayo yalisemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipokuwa akijibu maswali kadhaa yaliyoulizwa na baadhi ya wahariri, aliokuwa akizungumza nao, katika ziara aliyofanya leo, katika Kampuni ya New Habari Corporation, Sinza jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahariri, waliohoji ni kwa nini CCM haijitokezi kumpongeza Dk. Magufuli katika juhudi ambazo ameanza kuonyesha katika kupambana na ufisadi ikiwemo kubana fedha za walipa kodi ambazo zingepotea bure katika masuala yasiyo ya lazima na wakati huohuo kuanza kuwabana wafanyabiashara wanaodaiwa kukwepa kulipa ushuru.
"Yapo mengi tuliyoanisha katika ilani yetu ya Uchaguzi, na yote yahahusiana sana na haya mnayoyaona yanafanywa na Rais Dk. John Magufuli, tena Ilani hii tumeitunga hata kabla ya kumteua kugombea Urais, Sasa anachofaya ni kuitekeleza ilani hii, isipokuwa mbinu anazotumia ni ubunifu wake na hili hatuna tatizo nalo kama Chama maana kiongozi wa aina hii ndiye tuliyemtaka", alisema Nape.
"Najua wapo wanaojaribu kutengeneza magingira ya kumtaka kumtenganisha Dk. Magufuli na CCM, nawambieni Dk. Magufuli ni zao la CCM na mwana CCM Kindakindaki, hivyo ni upotoshaji wa hali ya juu kujaribu kuuaminisha umma kwamba anayofanya Dk. Magufuli hayana uhusiano na maelekezo ya CCM", aliongeza Nape.
Alisema, baada ya kutengeneza ilani yake, CCM, ilidhamiria kwamba, awamu hii ya tano ni ya kutafsiri uchumi katika nyanja za huduma za Jamii, ikiwemo miundomboni, maji, afya na elimu.
"Ni kutokana na lengo hili, ndiyo sababu tukakaa kwa makini na kuhakikisha ilani hii ya sasa tunamkabidhi mwana CCM ambaye utekelezaji wake hautakuwa wa mashaka mashaka, Ndiyo huyo Dk. Magufuli, bila shaka sasa na ninyi ni mashahidi mmeanza kuuona utekelezaji wake wa ilani", alisema Nape.
Akizungumzia kuhusu Rais Dk. Magufuli kuchelewa kutangaza Baraza lake la Mawaziri, Nape alisema, Chama Cha Mapinduzi kimeshaunda serikali kwa kumpata Rais, kilichobaki sasa ni kwa Rais mwenyewe kuteua watendaji wake, lakini katika kufanya hivyo hakuna mda aliopangiwa kuanza kufanya hivyo na hashurutishwi na Chama wala sheria.
Nape alisema, Dk. Magufuli hachelewi kuteua Baraza la Mawaziri kwa sababu anakosa wakuwateua, isipokuwa, anayo namna na mda ambao mwenyewe Kama Rais amejipangia, na mda huo ukijiri wa kuamua kufanya hvyo atafanya.
"Tatizo hapa ni kwamba mnayo kiu kubwa ya kutaka kujua nani atawateua, sasa kiu yenu imepita kiasi, ndiyo maana mnaanza kuhoji, lakini mimi naamini Dk. Rais Magufuli ataikata kiu yetu, wala msipate taabu ya kuhoji kila kukicha", alisema Nape.
Nape alisema, mbali na Chama kutengeneza ilani ambayo italeta mageuzi makubwa ya kiuchumi hapa nchini, pia Watanzania watarajie kuona mageuzi makubwa ndani ya CCM, kwa sababu yapo njiani kuwadia.
"Kama ilivyo kawaida yetu, kila baada ya uchaguzi mkuu huwa tunafanya tathmini, baada ya tathmini hiyo, huwa lazima tufanye mageuzi kwa yale ambayo tumebaini kuwa ni kikwazo kwa uhai na maendeleo ya Chama katika nyanja mbalimbali, na mageuzi haya tunayafanya kuzingatia mahitaji ya sasa na wakati ujao", alisema Nape.
Kuhusu Mwenyekiti wa sasa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kumwachia Ueneyekiti Rais Dk. Magufuli, Nape alisema, hayo si mambo mageni kwa CCM, imekuwa ikifanyika katika awamu zote za Urais, hivyo Kikwete anaweza akaamua kumwachia kabla ya uchaguzi mkuu wa CCM utakaofanyika mwaka 2017 au kabla ya hapo akiona inafaa.
Zanzibar
Akizungumzia mgogoro wa Zanzibar uliotokana na kufutwa uchaguzi mkuu wa Rais wa Zanzibar, Nape alikiri kamba ni mbaya na unaitia doa Tanzania, akisema, lakini akasisitiza kwamba njia pekee ya kuumaliza ni kwa mazungumza baina ya viongozi wa ndani bila kushirikishwa mataifa ya nje.
Alisema, msingi wa mgogoro uliojitokeza Zanzibar, si wa kisheria, bali ni wa kisiasa zaidi, hivyo juhudi ziwekwe kwenye mazungumzo kuutatua, na baada ya kuutatua yaendelee kufanyika mazungumzo ambayo yataleta suluhisho la kudumu kwa kuwa imekuwa ni kawaida kwa Zanzibar kuzuka migogoro kila baada ya uchaguzi mkuu jambo linaloonyesha kuwa tatizo ni la asili zaidi kuliko inavyodhaniwa.
Katika mazungumzo yake na wahariri hao wa New Habari Corporation Ltd, Wachapishaji wa magazeti ya Rais, Mtanzania na Dimba, alivitaka vyombo vya habari nchini, sasa kushirikiana na Serikali kulijenga taifa.
"Tunajua wakati wa kampeni kulikuwa na mambo mbalimbali ambayo wakati mwingine vyombo vya habari vililazimika kukampenia vinaowaona kuwa wanafaa kutokana na sababu mbalimbali, lakini kama tulivyokuwa tukisema, kwamba baada ya uchaguzi maisha yataendelea, sasa umefika wakati wa kuendelea na maisha tuwe kitu kimoja", alisema Nape.
Alivitaka vyombo vya habari, kusaidia kuishari Serikali na CCM, katika kutekeleza yaliyo bora kwa taifa na hata pale vyombo hivyo vitakapoona kwamba Chama au serikali vinaenda kinyume, visihofii kukosoa.
Kwa upande wao, Mtariri Mtendaji wa Habari Corporation, Absalom Kibanda akimpongeza Nape kwa ushirikiano ambao amekuwa akivipa vyombo vya habari, na kumtaka aendelee kuwacha milango wazi kwa waandishi wa habari kama ambavyo amekuwa akifanya.
Ziara hiyo ya Nape aliyoianza jana, kwenye vyombo vya habari inatarajiwa kuendelea kesho kwa kutembelea vyombo vingine vya habari vyenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam.

Tanzania’s new President, John Magufuli, inspires new Trend

Written by Omar Mohammed for Quartz
This Post First Appeared on Quartz

UPANUZI WA BARABARA YA MWENGE-MOROCCO DAR WAANZA

 Mafundi wakiendelea na upanuzi wa Barabara ya Mwenge-Morocco jijini Dar es Salaam leo, ikiwa ni sehemu agizo la Rais Dk. John Magufuli, ambaye alielekeza fedha za maadhimisho ya Siku ya Uhuru Desemba 9, mwaka huu, zitumike katika upanuzi wa barabara hiyo yenye urefu wa Km 4.3.(NA MPIGAPICHA WETU)

UJENZI WA KISIWA CHA KITALII WAANZA KATIKA ENEO LA MTONI MARINE KASKAZINI MAGHARIBI ZANZIBAR

 Sehemu  inayoendelea kufukiwa hapo Mtoni Marine ambayo itatumika hapo baadae kwa ajili ya eneo maalum litakalotoa fursa kwa Wananchi  kupata mapumziko.{ Public Beach }. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar { ZIPA } Nd. Salum Khamis Nassor  akimueleza Balozi Seif  hatua zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kuona taratibu za uwekezaji zinachukuliwa kwa wanaowekeza vitege uchumi vyao Nchini. 
Balozi Seif akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baghresa Group Bwana Said Salim wakitembelea kuona  mradi wa Ujenzi wa Majengo Mapya ya Hoteli ya Mtoni Marine ambayo iko chini ya Kampuni hiyo kwa hivi sasa.

MRADI mkubwa wa Kimataifa wa ujenzi wa kisiwa cha Kitalii  ambacho kitatengenezwa kwa mfumo wa ufukiaji Bahari umeanza rasmi katika eneo la Hoteli ya Utalii iliyopo Mtoni Marine kaskazini Magharibi ya Mji wa Zanzibar.

Hata hivyo gharama kamili za Mradi huo bado hazijafahamika  wakati utakapokamilika  rasmi ujenzi wake hapo baadaye.

Mradi huo unaoendeshwa na Kampuni ya Kizalendo  ya Baghresa Group utahusisha ujenzi wa Hoteli ya Kimataifa ya Ghorofa  Tano ya Daraja la Tano { Five Star + }, utengenezaji wa eneo la wazi la mapumziko { Public Beach } pamoja na kutengeneza  Kisiwa cha Mji mpya.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alishuhudia harakati za ujazaji wa mchanga katika eneo linalofukiwa ambazo hufanywa kwa utaalamu wa hali ya juu.

Mhandisi wa Mradi huo Bwana Ahmed Shamsi alimueleza Balozi Seif  kwamba chombo maalum kinachotumika kwa kazi ya uchimbaji wa mchanga Baharini  kina uwezo wa kunyonya  na kusafirisha mchanga kutoka ndani ya Bahari sambamba na kukata Majabali.

Mhandisi Shamsi alisema kazi hiyo inafanyika kwa saa 12 kila siku ambapo takwimu zinaonyesha wazi kwamba uchimbaji huo wa mchanga unaokwenda  zaidi ya mita 15 chini ya Bahari unafikia  Tani 600 za mchanga kwa saa Moja.

Alifahamisha kwamba harakati za uchimbaji na kufukia mchanga katika eneo hilo zilizoanza Mwezi uliopita wa Novemba zinatarajiwa kukamilika mwezi Januari mwaka ujao.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baghresa  Group  Bwana Said Salim Baghresa alisema kwamba ujenzi wa mradi huo muhimu kwa uchumi wa Nchi utasaidia mapato ya Taifa pamoja na kutoa ajira kubwa kwa vijana Wazalendo hapa Nchini.

Bwana Baghresa alisema mfumo wa ufukiaji Bahari kwa ajili ya kuanzisha miradi ya Kiuchumi ni mfumo unaotumiwa na Mataifa mbali mbali Duniani ambapo kwa Afrika  mradi kama tayari umeanza kutumiwa katika Kisiwa cha Seycheles.

Akitoa nasaha zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameupongeza Uongozi wa Baghresa Group kwa uamuzi uliochukuwa wa kuanzisha mradi huo mkubwa wa Kimataifa.

Balozi Seif alieleza kwamba kukamilika kwa mradi huo mkubwa  ambao umeshazoeleka katika Mataifa yaliyoendelea utasaidia kuitangaza Zanzibar na Tanzania kwa ujumla  Kiutalii Kimataifa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia Uongozi huo wa Baghresa Group kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatoa kila msaada unaohitajika katika  kuona mradi huo unafikia malengo uliojipangia.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamui wa Pili wa Rais wa Zanzibar
1/12/2015.

MAKONTENA YALIYOTOROSHWA BILA KULIPIWA BANDARINI YANASWA MBEZI

 Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo, akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo ambalo yalikutwa makontena tisa Mbezi Tangi bovu, ambayo hayajafahamika yamewekwa kitu gani na mmiliki wake hajajitokeza.

WAZIRI MKUU MSTAAFU AMKABIDHI RASMI OFISI WAZIRI MKUU MAJALIWA


 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimkaribisha  Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda  ambaye Novemba 30,2015 alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kukabidhi Ofisi.
  Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo  Pinda ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015 kukabidhi Ofisi. 
 Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda wakimsikiliza  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Florence Turuka aliposoma taarifa kabla ya Waziri Mkuu Mstaafu kukabidhi Ofisi, kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015.
  Waziri Mkuu, Mstaafu Mizengo Pinda  akizungumza  kabla ya kukabidhi Ofisi kwa  Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa,  kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015.
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa  akipokea taarifa ya makabidhiano ya Ofisi ya Waziri Mkuu kutoka kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuujijini Dar es salaam Novemba 30, 2015. 
 Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea taarifa ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Waziri Mkuu Mtaafu, Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Maka  Kikula. 
 Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea taarifa ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Waziri Mkuu Mtaafu, Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 215. Watatu Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Maka  Kikula.
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akifurahia  katika mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo  Pinda  na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florence Turuka baada ya Waziri Mkuu Mstaafu kukabidhi rasmi Ofisi ya Waziri  kwa  Waziri  Mkuu Majliwa , kwenye ukumbi wa Ofisiya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MAJALIWA AKUTANA NA MABALOZI WA CHINA, KOREA NA SUDAN


 Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na balozi wa China Nchini Dkt. Lu Youqing kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es slaam  Disemba 1, 2015. 
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Sudan nchini, Dkt.Yassir  Mohamed Ali Ofisini kwake jijini Dar es salaam Disemba 1, 2015.
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa   akisalimiana na balozi wa Sudan nchini,Dkt. Yassir Mohamed Ali kabla ya mazungumzo yao Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Disemba 1, 2015.
 Waziri Mkuu,Majaliwa Kassim Majliwa akizungumza na balozi wa Korea nchini Mhe. Chung Il ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Disemba 1, 2015 kuaga.
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kinyago balozi wa Korea nchini, Mhe. Chung Il ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 1, 2015 kuaga.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

JAJI MAKURU AFUNGUA MAFUNZO MAALUM YA HUDUMA KWA WATEJA KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA YA TANZANIA.


 Elizabeth J. Kisamba, (aliyesimama), mshiriki toka Mahakama ya Wilaya Temeke Dar es Salaam, akichangia mada katika mafunzo ya Huduma kwa wateja, yaliyofanyika mkoani Dodoma.
 Praxeda S. Joseph, (aliyesimama), mshiriki toka Mahakama Kuu Tabora, akifafanua jambo juu ya mada iliyotolewa katika kuboresha huduma kwa wateja mahakamani.
 Watumishi wa Kada mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania waliohudhuria mafunzo ya Huduma kwa wateja ili kuweza kuwajengea ujuzi na ufanisi katika kazi mahakamani.
 Simon Berege, Mwenyekiti wa MISA-TAN Afrika, akielezea umuhimu wa mafunzo ya huduma kwa wateja hasa kwa watumishi wa Mahakama ili kuweza kutoa taarifa sahihi ambazo zitarahisisha  kutoa haki na kwa wakati.
 Bw. Nurdin Ndimbe, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mahakama ya Tanzania, akitoa risala fupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mafunzo ya Huduma kwa Wateja kwa Watumishi wa Mahakama ya Tanzania. 
 Mhe. Jaji Crescencia Makuru, Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, akifungua rasmi mafunzo maalumu ya Huduma kwa Wateja kwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania, leo mkoani Dodoma. 
Mhe. Jaji Crescencia Makuru, Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, (aliyeketi wa pili toka kushoto), Nurdin Ndimbe, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mahakama ya Tanzania, (wa pili kulia), Deus Kibamba, Mkurugenzi wa TCIB, (wa kwanza kulia), Simon Berege, Mwenyekiti wa MISA-Tanzania, (wa kwanza kushoto), katika picha ya pamoja na Watumishi wa Kada mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania washiriki wa mafunzo ya Huduma kwa Wateja,                                                                 Mkoani Dodoma.                                                                                                                                                                     
MAFUNZO maalumu ya siku mbili yahusuyo huduma kwa wateja na haki ya kupata taarifa kwa watumishi wa Mahakama, yamemalizika leo katika hoteli ya St.Gaspar mjini Dodoma.

Akifungua rasmi mafunzo hayo  Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, Mhe. Crescencia Makuru, amesema moja ya malengo makuu ya mafunzo hayo, ni kuwajengea uwezo watumishi wa Mahakama kwa kuwapa mbinu na mikakati mbalimbali itakayowasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

“Mahakama ya Tanzania kwa sasa inaendelea na maboresho ya utendaji kazi wake kama sehemu ya kuhakikisha kuwa inatoa huduma iliyo bora na kwa wakati”, Jaji Makuru amebainisha.

Mwaka 2014 Mahakama ya Tanzania kama moja ya Taasisi ya Serikali ilifanyiwa tathmini kuhusu utoaji wa haduma zake hasa katika nyanja ya upatikani na utoaji wa taarifa kwa Umma iliyoendeshwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, (Media Institute of Southern Africa-MISA). 

Katika tathmini ile, Mahakama ilikuwa ya mwisho na ilizawadiwa kufuli la dhahabu kama alama ya kuonyesha kuwa taasisi hii ni moja kati ya zilizojifunga sana kutoa taarifa kwa wananchi. Moja ya maeneo yaliyoonekana na udhaifu ni namna masijala za Mahakama zinavyopokea na kutunza nyaraka na hata wanavyowahudumia wateja kwa ujumla.

Mafunzo hayo endelevu yamelenga kuwafundisha makarani na watumishi wa kada mbalimbali nini maana ya uhuru wa Habari na habari ni Nini?, Huduma kwa wateja na ujuzi wa mawasiliano kwa watumishi wa Umma , Njia mbalimbali za upatikanaji wa taarifa katika Taasisi za Umma na Sheria ya utoaji wa  habari katika Mahakama.

Mafunzo haya yameandaliwa na kufadhiliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) pamoja na Taasisi ya Friedrick Ebert Stiftung (FES) ofisi ya Tanzania.

Wanaotembelea Blogu hii