Afisa
Utumishi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, ambaye alimwakilisha
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna
akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani katika kupitisha sheria ndogo ya
Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini
wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha mwisho kimefanyika Machi 29,
2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni
Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya
Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera (kulia), Makamu Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga, Mheshimiwa
Francis Komba (kushoto).
Meneja wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally
Mwakababu akitoa maelezo machache juu ya TIKA. Pembeni ni Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga,
Mheshimiwa Francis Komba na Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe
ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera.
Wajumbe wa Baraza la Madiwani wakifuatilia kwa makini.
Comments