Usiku wa jana haukuwa mzuri kabisa kwa meneja wa mashetani
wekundi ‘David Moyes’ baada ya kikosi chake kukubali kipigo cha bao 3 –
1 kutoka kwa wenyeji wao, timu ya Bayern Munich ya Ujerumani.
United ndio waliotangulia kupata goli la kwanza kupitia
beki wake ‘Patrice Evra’ mnamo dakika ya 57′ ya kipindi cha pili cha
mchezo.
Hapa
ni ule wakati wa benchi la ufundi la United wakiongozwa na kocha Moyes
wakishangilia bao la kwanza alilofunga Evra. kweli kutangulia sio
kufika.
Hata hivyo hali ya mchezo ilibadilika ghafla baada ya mshambuliaji wa Munich ‘Mario Mandzukic’ kusawazisha dakika ya 59′ na kisha kufuatiwa na Thomas Muller aliyefunga goli la pili dk 68′ kabla ya kijana mzee ‘Arjen Robben’ kufunga bao la tatu dakika ya 76 na kuifanya timu yake kufuzu hatua ya nusu fainali.
Ribery akimpongeza Arjen Robben baada ya kupachik.a bao la tatu
Furaha
ilipofikia mwisho wake, Kocha wa United ‘Moyes’ akifuta machozi huku
akishuhudia vijana wake wakisulubiwa goli 3 na wajerumani.
Mchezo mwingine uliokuwa wa patashika nguo kuchanika ni ule
uliozikutanisha timu mbili za hispania, Atletico Madrid na Barcelona,
ambao ulimalizika kwa Atletico kuibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya
Barca kupitia mchezaji wao Koku dakika ya 5 na hivyo kujitwalia jumla
ya pointi 6 na magoli 3 – 1 dhidi ya Barcelona katika michezo miwili
waliyocheza na kufuzu hatua ya nusu fainali.
Comments