BOMU LALIPUKA NA KUJERUHI WATU KWENYE BAR JIJINI ARUSHA.

ArushaMlipuko mkubwa umetokea hapo jana majira ya saa 1.30 usiku katika baa maarufu ya Arusha night park iliyopo eneo la Mianzini mjini Arusha na kujeruhi watu waliokuwepo eneo hilo.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa mlipuko huo ulitokana na bomu lililotengwa katika eneo la bar hiyo na kujeruhi watu zaidi ya 20 waliokuwa wakiangalia mechi kati ya Chelsea na Swansea.
Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya dk. Mohamed na Mount Meru. Mashuhuda wanaeleza kuwa kuna baadhi ya majeruhi wamekatika viungo kama miguu nakadhalika.
Hili ni tukio la tatu mjini arusha bomu kurushwa na kutegwa katika maeneo ya mikusanyiko ya watu ambayo ilipelekea kujeruhi na kupoteza maisha ya watu.
Arusha1 Arusha2 Arusha3
Mlipuko ArushaPichani ni sehemu ambayo mlipuko ulitokea.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU