Marafiki wa kweli utawajua pale
unapopatwa na matatizo, Mama mzazi wa Chris Brown ‘Joyce Hawkins’
aliyekuwa ameambatana pamoja na mkwe wake ‘Karrueche Tran’, Rapa Bow Wow
na Tank wameonekana kwenye viunga vya mahakama jijini Washington DC
ikiwa ni katika hali ya kumpa kampani jembe lao.
Mchumba
wa Chris Brown ‘Karrueche Tran’ (Wa kwanza kushoto) akiingia mahakamani
pamoja na mama mzazi wa Brown ‘Joyce Hawkins’ aliyevalia koti jeusi.
Mkali huyo anayesumbua na ngoma ‘Loyal’ ambaye kwa sasa
anatumikia kifungo cha mwezi mmoja gerezani kufuatia makosa ya uvunjaji
sheria aliyoyafanya pindi alipokuwa Rehab.
Hata hivyo jaji aliyekuwa akitarajiwa kutoa uamuzi dhidi ya
kesi hiyo kwa mlinzi wake ‘Christopher Hollosy’ siku ya Ijumaa
alichelewa na kesi kuahirishwa hadi jumatatu. Kesi ya Chris itaanza
kusikilizwa Jumatatu.
Bow Wow akiwasili mahakama kumpa sapoti mshikaji wake huyo wa kitambo kirefu
Karrueche Tran
Mwanamuziki Tank nae alikuwa miongoni mwa watu waliojitokeza mahakamani kumpa kampani Brown.
Comments