DIAMOND AZIDI KUPETA TUZO ZA KORA.

Mwanamuziki Diamond Platnumz ameandika leo kupitia ukurasa wake wa Facebook akiwashukuru watanzania na wapenzi wa muziki wake wanaoendelea kumpigia kura kwa ajili ya  kumuwezesha kunyakua tuzo kubwa za Afrika  ‘KORA’ ambazo hufanyika mara moja kwa mwaka.
Diamond Platnumz Nigeria
Tuzo hizo zinawapa nafasi mashabiki ya kuwapigia kura kwa njia ya  mtandao wasanii wanaowaona  wanastahili kushinda kwa njia ya kulike ukurasa wa Kora kisha kulike katika kila posti utakayoona picha au jina la msanii  unayemkubali.
Wiki hii Diamond ameweza kupata kura zilizoweza kumtoa nafasi ya 14 wiki iliyopita mpaka nafasi ya tatu kwa wiki hii ikiwa ni  kwa Afrika nzima.  Amr Diab, Koffi Olomide, Fally Ipupa, Werrason, Mafikizolo  ni baadhi ya wasanii waliopo kwenye kinyang’anyiro kimoja na rais wa watu wasafi ‘Diamond’.
Kora
”Hakika nimeamini Umoja ni nguvu, na tukizidi kushirikiana mziki wetu utazidi fika mbali na kuleta heshima na sifa zaidi nyumbani… Kutoka nafasi ya 14 katika tunzo za Kora wiki ilopita hadi leo kushika nafasi ya 3 Africa Nzima… kiukweli ni hatua kubwa sana, na nawashkuru sana sana… tafadhari naomba kwapamoja mnipigie kura tena na hatimaye tushike nafas ya kwanza na hadi kutwaa kabisa….JINSI YA KUPIGA KURA: unaingia katika link hii hapo chini kisha unalike page ya Kora Awards kisha katika kila Post utayoona jina au Picha yangu Unacomment kwa kuandika Jina langu Diamond Platnumz… hapo utakuwa umeniwezesha… kama ushalike page usiilike tena, Ahsante!” Aliandika Diamond…

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*