DUDUBAYA AKANUSHA VIKALI KUMKATA SIKIO MAMA YAKE.


DuduBayaMwanamuziki nguli wa muziki wa kufokofoka nchini Tanzania, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ amekanusha vikali tuhuma zinaendelea kusambaa kama moto wa kifuu kuhusu kumkata sikio mama yake mkubwa huku akidai kwamba wanaosambaza maneno hayo ni ndugu zake wa damu kabisa ambao wanamuonea wivu kufuatia kitendo chake cha kumjengea nyumba mama yake mzazi.
”Nashangaa sijapigiwa simu na sijua kama kuna tukio gani ama nini. Unajua hivi vitu sivielewi, mimi nawasiwasi  hii inshu na ndugu zangu binafsi. Ndugu zangu walikuwa wakiongea maneno kibao mara Dudubaya hajajenga  kwao kisesa.  Kwa hiyo ni ndugu ambao hata kwenye hili suala wanajaribu kukrieti vitu flani kwamba huyu kafanya hivi kumkata sikio mama yake mkubwa ili kunichafulia katika jamii nionekana namna gani” alisema Dudubaya alipokuwa akifanyiwa mahojiano na Soudy Brown ‘Gossip Cop’.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI