Jarida marufu Duniani la Forbes ambalo hutoa orodha ya watu
matajiri zaidi Duniani kila mwaka, kwa mara nyingine tena limetoa
orodha ya wasanii watano matajiri wanaofanya muziki wa kufokafoka ‘Hip
Hop’.
Katika orodha hiyo Sean Combs ei kei ei Puffy Daddy ndiye anaongoza katika orodha hiyo kwa kuwa msanii tajiri kwa mwaka huu.
Utajiri wake unakadiriwa kufikia kiasi cha dola za
kimarekani milioni 700 ukiwa umeongezeka kiasi cha dola milioni 120
toka mwaka jana. Hiyo ni kutokana na televisheni yake ya REVOLT pamoja
na mvinyo anaoutengeneza wa CIROC na kampuni zake nyingine kama vile BAD
BOY ambavyo vimechangia kwa kiasi kikumbwa kumuweka kileleni.
Akifuatiwa na producer Andre Romelle Young AKA DR.Dre
akiwa na utajiri unaofikia dola milioni 550, huku utajiri wake
ukitokana na mauzo ya Headphones zake za BEATS BY DRE sambamba na mziki
anaozidi kuufanya.
Katika nafasi ya tatu anakaa mtu mzima Sean Carter ‘Jay Z’
au unaweza kumuita baba Blue Ivy akiwa na utajiri wa kiasi cha dola
milioni 520 huku vyanzo vya utajiri huo vikitajwa kuwa ni kampuni yake
ya mavazi ya Roca Wear, Live Nation pamoja na Roc Nation.
Wakati nafasi ya nne ikikamatwa na Bryan Adams al maarufu
kama BIRDMAN huku utajiri wake ukitokana na CASH MONEY, YMCMB na GTV
Vodka akiwa na utajiri wa milioni 160.
Na aliyeshikilia nafasi ya tano ni Curtis Jackson maarufu kwa
jina la jukwaani 50 Cent akiwa na utajiri wa milioni 140, vyanzo vya
mapato yake vikitajwa kuwa ni maji yake anayoyauza ‘VITAMIN WATER’, SMS
AUDIO Headphone na SK Energy
Comments