Jumuiya ya Watanzania nchini Malaysia yapata Uongozi wao

Jumamosi ya tarehe 29 March 2014, watanzania waishio na wasomao Malaysia walikutana katika Ubalozi wa Tanzania na kuunda Jumuiya mpya ya Watanzania wanaoishi South East Asia.

Uongozi wa Wana Jumuiya hiyo ambao kwa kuanzia ni Watanzania waliopo Malaysia wakiwa na Balozi Mpya wa Tanzania,Dr. Aziz Ponary Mlima (katikati) na maafisa wa Ubalozi. Viongozi waliochaguliwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Katibu Mkuu, Waziri wa Fedha, Waziri wa Elimu, Waziri wa Jamiii, Utamaduni na Starehe ikiwa pamoja na Wadhamini wawili.
Picha nyingine ni Watanzania wote kwa pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi na Balozi Mpya wa Tanzania nchini Malaysia.

Jumuiya hiyo ilianzishwa Mwishoni mwa wiki,ambayo inajulikana kama " Tanzanian Diaspora in South East Asia"  ambayo itakuwa inawashirikisha Watanzania wote katika nchi za Malaysia, Indonesia, Thailand, Philippines, Brunei, Laos na Cambodia.

Picha zaidi zinaweza kuonekana kwenye Ukurasa wa Facebook


Watanzania kutoka maeneo hayo wanaombwa kujiunga ili tuweze kutambuana na itakapokuwa lazima kusaidiana.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.