Hawa
Ladha meneja miradi Serengeti breweries, Bw Evans Mlelwa meneja
mawasiliano serengeti breweries na Bw Joseph Mkirikiti Mkuu wa Wilaya
Songea wakizindua miradi ya maji Songea iliyogharimu zaidi ya millioni
140 hivi karibuni.
Kampuni
ya Bia ya Serengeti Breweries kupitia mpango wake wa kusaidia
jamii,imekabidhi rasmi mradi wa maji uliopo katika Kituo cha afya cha
Mletele na kituo cha afya cha Tanga vilivyopo mjini Songea. Mradi huo
umezinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya Mh. Joseph Mkirikiti ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo
Mradi
huo wa maji ambao umegharimu zaidi ya Shilingi milioni 140 za kitanzania
unatarajia kukidhi mahitaji ya watu zaidi ya 100,000 wanaohudumiwa na
vituo hiyo na jamii inayovizunguka.. Miradi hii kwa kiasi kikubwa
utapunguza mfumuko wa magonjwa na vilevile vifo vya watoto na kina mama
wajawazito.
Mradi
wa Hospitali ya Mletele unajumuisha kisima , pampu ya maji ya solar na
matanki ya kuhifadhia maji ya lita elfu kumi, na mradi wa Na mradi wa
maji wa Hospitali ya Tanga unajumuisha kisim na pampu ya maji ya solar.
Visima hivi viwili vinaweza kutoa lita 72,000 kwa siku.
Akiongea
katika hafla fupi hospitalini Mletele , Bw. Mkirikiti amesema “
Nafarijika sana kuona hospitali hii sasa imepata suluhisho la tatizo la
maji walilokuwa nalo hapo awali. Ningependa kuwashukuru sana Serengeti
Breweries kwa juhudi zao katika kusaidia shughuli za kijamii na hasa
katika upatikanaji wa maji safi na salama na hasa katika hospitali
zetu.”
Kampuni
ya Bia ya Serengeti wamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia
upatikanaji wa maji safi na salama na tayari wamewezesha miradi
mbalimbali ya maji kama vile Iringa – Hospitali ya Frelimo, Moshi –
Hospitali ya Mawenzi, Dares salaam – Hospitali ya Temeke na ule wa
Mkuranga na Sekou Toure mwanza.
Mkurugenzi
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti , Bwana
Evans Mlelwa , amesema “Suala la kuisaidia jamii kwa Kampuni ya Bia ya
Serengeti limepewa kipaumbele na uzito wa hali ya juu na hasa katika
kusaidia upatikanaji wa maji safisalama na pia endelevu.
Serengetti
Breweries inatambua umuhimu wa maji kwa binadamu na pia mchango wa maji
katika maendeleo ya nchi, kiuchumi na kijamii. Tutahakikisha
tunaendelea kuwekeza katika miradi ya maji kwa ajili ya jamii
inayotuzunguka ili kuongeza ari ya uwajibikaji kwa maendeleo ya taifa
letu na kwa ustawi wa kila mmoja wetu”,ameongeza Bw. Mlelwa.
“Kampuni
ya Bia ya Serengeti na EABL Foundation mpaka sasa tumeshawekeza zaidi
ya milioni 500 za kitanzania , katika maeneo mbalimbali ambapo zaidi ya
watu 450,000 wanafaidika na miradi hiyo”.
Comments