KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI KATAVI

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa Afisa Zana za Kilimo wa Wilaya ya Mlele,kuhusiana na Mradi wa Mashine ya Kusindika Mpunga mapema leo jioni,katika kijiji cha Mwampuli,Wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi,Mashine hiyo ina uwezo wa kusindika mpunga tani 30 kwa siku.Kushoto ni Mjumbe wa NEC Taifa,Balozi Ali Karume nae akisikiliza kwa makini.Kinana yupo Mkoani Katavi kwa ziara ya siku nne ya kuimarisha uhai wa chama,kukagua na kuhimiza ilani ya Uchaguzi ya 2010.
Mradi wa Mashine ya Kusindika Mpunga kama uonekavyo pichani uliopo katika kijiji cha Mwampuli,Wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi,Mashine hiyo ina uwezo wa kusindika mpunga tani 30 kwa siku.
Katibu Mkuu wa CCM,akikagua Ujenzi wa Mradi wa Maji safi,katika kijiji cha Kibaoni,Wilaya ya Mlele,mkoani Katavi.Tanki hilo la maji safi linatarajia kuhudumia wakazi wa kijiji cha Kibaoni na vijiji vingine tisa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wa tatu kulia akishiriki kukusanya mawe pamoja na viongozi mbalimbali wa Taifa,Mkoa na Wilaya (CCM),kukusanya mawe kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa shule ya msingi Maji Moto iliyopo katika kijiji cha Maji Moto,Wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Maji Moto jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara,Nape amewataka wana CCM na wananchi kwa ujumla kuishi kwa amani na upendo katika suala zima la kudumisha amani tulionayo na kuwapuuza wanaotaka kuleta mgawanyiko katika nchi yetu kwa namna moja ama nyingine.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Maji Moto jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara,Kinana ameeleza kuwa kumekuwepo tatizo kubwa kila mahali aendapo kufanya ziara kuhusiana na migogoro ya ardhi kati ya Wakulima na Wafugaji,Wafugaji na Hifadhi,jambo ambalo linapaswa kufanyiwa kazi kwa umakini mkubwa sana,aliongeza kuwa migogoro hiyo imekuwa janga la Taifa,kutokana na idadi ya watu kuongezeka katika maeneo mengi,huku mipaka yake kubaki kama iliyo kwa muda mrefu.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mama Mzazi wa Waziri Mkuu,Mh Pinda, mapema mchana huu nyumbani kwake,Katika kijiji cha Kibaoni Wilaya Mlela mkoani Katavi,alipokwenda kumtembelea na kumjulia hali.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Mama Mzazi wa Waziri Mkuu,Mh Pinda, mapema mchana huu nyumbani kwake,Katika kijiji cha Kibaoni Wilaya Mlele mkoani Katavi,alipokwenda kumtembelea na kumjulia hali.Kinana yuko Mkoani Katavi kwa ziara ya siku nne ya kuimarisha uhai wa chama,kukagua na kuhimiza ilani ya Uchaguzi ya 2010.
Kinana akijaribu kuelewesha jambo katika shamba la Ufugaji nyuki la Waziri  Mkuu Pinda,katika kijiji cha Kibaoni Wilaya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo mchana.
Kinana akikatiza kwenye Shamba la Ufuta na Nyuki mara baada ya kujionea ufugaji wa nyuki unavyofanyika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA