KATIBU MKUU WA CCM,KINANA ATEMBELEA MJI WA KIHISTORIA WA UJIJI,AKUTANA NA WAVUVI WADOGO WADOGO ZIWA TANGANYIKA


 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi ndani ya Nyumba ya Makumbusho ya Dr Livingstone iliyopo katika eneo la Ujiji mkoani Kigoma 
 Katibu Mkuu wa CCM (tatu kulia),Ndugu Kinana pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM,Mkoa na Wilaya wakipata maelezo mafupi kuhusiana na historia ya mnara huo,ambao Dr.Livingstone na Henry M.Stanley walikutana kwa mara ya kwanza katika mji wa Kihistoria wa Ujiji mkoani Kigoma katika suala zima la kusambaza dini na kupambana na biashara ya Utumwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akisalimiana na Mama Mawazo Rashid Mawala mkazi wa Ujiji Kigoma ,Katibu Mkuu alikuwa akitembea kwenye njia (route) iliyotumika na Watumwa ambapo kuna miembe yenye umri zaidi ya miaka 150,miembe kama hii inapatikana sehemu ya ya Tabora na Bagamoyo. 
 Sehemu ya njia (route) kama ionekanavyo pichani ndani mji wa kihistoria Ujiji mkoani Kigoma,iliyotumika kusafirishia Watumwa kwenda sehemu mbalimbali,katika njia hiyo kuna miembe inayoelezwa ina umri zaidi ya miaka 150 tangu kupandwa kwake,na inaelezwa inapatikana sehemu ya Tabaro na Bagamoyo. 
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mzee Masoud Mwinyi Chande kwenye mnara wa kumbukumbu ya nyumba ya kwanza ambayo Mwalimu Julius Nyerere alifikia Ujiji wakati akifanya harakati za kutafuta Uhuru, Inaelezwa kuwa Nyumba hiyo Mwalimu Nyerere alifika akiongozana na Suleiman Takadili na Bibi Titi Mohamed.Kulia ni Mbunge wa Kigoma Mjini,Mh Peter Serukamba,Katibu wa NEC,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye,pamoja na Mwenyekiti wa CCM-Kigoma Ndugu Amani Kabouru.

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akielekezwa sehemu ya Chumba na mlango ndani ya nyumba ya kwanza ambayo Mwalimu Julius Nyerere alifikia Ujiji wakati akifanya harakati za kutafuta Uhuru, Nyumba hiyo inasemekana Mwalimu Nyerere alifika akiongozana na Suleiman Takadili na Bibi Titi Mohamed.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya na Mkoa,wakiwasilia kwenye Nyumba ya Makumbusho ya Dr Livingstone iliyopo katika eneo la Ujiji mkoani Kigoma na kujionea mambo mbalimbali ya kihistoria yaliyomo ndani ya jengo hilo. 
 Mmoja wa wakazi wa eneo la Kibiri,ambalo liko ufukweni kabisa mwa ziwa Tanganyika mkoani Kigoma,akibandika mabango yake yenye ujumbe wa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,alipokwenda kutembelea eneo hilo na kusikiliza kero mbalimbali za wavuvi wadogo wadogo.
 Baadhi akina Mama ambao ni wafanyabiasha wa samaki na dakaa pamoja na uvuvi wakiwa wamekusanyika wakimsubiri Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwa ajili ya kuwazisilisha kero zao mbalimbali ikiwemo tozo za kodi na ushuru mkubwa ikilinganishwa na kipato chao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma bango lenye ujumbe wa kulalamikia kodi kubwa  wanazotozwa wavuvi wadogowadogo wa Kibirizi,Kigoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kibirizi mkoani Kigoma ambao wanakilio cha kutozwa kodi kubwa, kuvamiwa na majambazi wakati wa shughuli zao za uvuvi.
 Katibu Mkuu,Ndugu Kinana akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Ofisi mpya ya CCM,kata ya KIbirizi.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza kwenye kikao cha Mabaraza ya Jumuiya zote (CCM) katika ukumbi wa Kibo Peak Club,Wilaya ya Kigoma mjini mkoani humo,ambapo Kinana walizungumza mambo mbalimbali ya kutekeleza na kuhimiza Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010,pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii.
Pichani Kati ni Mbunge wa Kigoma Mjini,Mh Peter Serukamba akieleza jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (shoto) wakati wakielekea kutazama Nyumba ya Makumbusho ya Dr Livingstone iliyopo katika eneo la Ujiji mkoani Kigoma,kulia ni a Katibu wa NEC,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI