KIFUSI CHAUA WATU WATATU KATIKA MACHIMBO YA KOKOTO JIJINI DAR ES SALAAM

Kuhusu wachimba kokoto waliofukiwa na kifusi Dar mchana wa leo april 4.
6Inasemekana watu watatu waliotambuliwa kwa majina ya Msagala,Jacob na Mhando ambao ni  wakazi wa Bunju jijini Dar es Salaam wamefariki dunia mchana wa April 04  baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba kokoto.

Watu hao walikua wakichimba kokoto hizo kwenye machimbo ya Mtanzania mwenye asili ya Kiasia aliyefahamika kwa jina la Kara Arjan machimbo yaliyopo eneo la Bunju-Mbweni Dar es salaam.

Taarifa inasema kuwa machimbo hayo yalishapigwa marufuku kutokana na watendaji wake kufanya kazi katika mazingira hatarishi ambapo wachimbaji hao wakiwa kazini,sehemu ya machimbo hayo iliporomoka na kuwafukia.

Picha za kwenye tukio ambazo zinaonyesha pia juhudi za watu wakiendelea na uokoaji pamoja na miili ya watu waliopoteza maisha.

5

1

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*