KINANA AHITIMISHA ZIARA YA SIKU 5 KIGOMA,AHUTUBIA KATIKATI YA MVUA, ALOWA CHAPACHAPA NA WANANCHI


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana nawananchi alipowasili kwenye mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara yake ya siku 5, Mwanga, Manispaa ya Kigoma, ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwapungia mkono wananchi alipokuwa akiingia kwenye mkutano huo wa hadhara.
 Mjumbe wa NEC CCM kutoka Zanzibar, Balozi Ali Abeid Karume akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Kigoma leo. ambapo alisisitiza wananchi kuunga mkono Muungano wa Serikali mbili.

 Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara huku akiponda vyama vya upinzani kwa tabia yao ya akila mara kupiga kelele bila kusaidia ujenzi wa miradi ya maendeleo nchini.

 Baadhi ya wananchi wakiwa wamejifunika kwa nguo ili wasilowe na mvua wakati Ndugu Kinana akihutubia katika mkutano huo
 Kinana (wa pili kulia) na viongozi wengine wa CCM wakiwa jukwaani wakinyeshewa mvua sambamba na wananchi wakati wa mkutano huo wa hadhara. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa NEC CCM, Balozi Ali Abeid Karume, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Dk. Walid Kaborou na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Peter Serukamba.
 Ndugu Kinana akihutubia huku mvua kubwa ikinyesha wakati wa mkutano huo
 Baadhi ya wananchi wakiwa wamejikinga mvua kwa viti huku wakiendelea kumsikiliza Ndugu Kinana
Kinana na viongozi wengine wakiondoka baada ya mkutano kumalizika huku wakiwa wamelowa chapachapa kutokana na mvua iliyokuwa inanyesha wakati wa mkutano huo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*