KINANA AIAGIZA SERIKARI KUMNYANG'ANYA TENDA MKANDARASI 'FEKI' WA GATI LA BANDARI YA KAREMA,MPANDA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwa na viongozi wengine wa chama na serikali akitoka kukagua ujenzi wa Gati la Meli la Karema, Ziwa Tanganyika, wilaya ya Mpanda Vijijini, mkoani Katavi wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM. Ni takribani miaka mitatu mkandarasi aliyepewa ujenzi wa gati hilo  ameshindwa kumalizia ujenzi. Kinana amesema Mkandarasi huo ambaye pia amepewa tenda ya kujenga gati zingine tatu katika mwambao mwa  ziwa hilo, anyang'anywe tenda na kupewa mwingine atakayemalizia ujenzi haraka lianze kufanya kazi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kinana akielezea kusikitishwa na kitendo cha mkandarasi wa gati hilo ambaye inadaiwa hana uwezo wa kufanya kazi hiyo kupewa tenda  hiyo.
 Kinana akipita kwenye nyasi baada ya kukagua gati hilo ambalo ujenzi haujakamilika kwa muda wa miaka mitatu
 Kinana (waili kulia) akijadiliana jambo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kuhusu ucheleweshashwaji wa ujenzi wa gati hilo.
 Kinana akizungumza kwenye simu na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe ujenzi wa gati ilo na hatima yake.
 Eneo la Karema lililo ufukweni mwa Ziwa Tanganyika, Wilaya ya Mpanda Vijijini, Mkoa wa Katavi.
 Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, akielezea mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu ujenzi wa vyumba vya maabara vya Shule ya Sekondari ya Kata ya Karema,
 Kinana akisaidiana na mafundi kupiga plasta vyumba vya maabara ya Shule ya Skondari ya Karema.Ujenzi wa maabara unatarajiwa kukamilika Jni mwaka huu.
 Kinana akihutubia mkutano wa hadhara baada ya kupewa taarifa ya ujenzi wa Mwalo wa wa Ikola wa kupokelea dagaa n samaki, kuwaanika kuwahifadhi na kuwauza. Mradi huo umejengwa Halmashauri ya Mpanda .
 Mwanachama wa Kata ya Karema, Msolomi Msolomi akiuliza maswali mbalimbali kwa Ndugu Kinana (kulia) wakati wa mkutano huo . Katikati ni Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Kinana (wa pili kuli)  akikagua eneo la kuanikia dagaa na samaki katika mwalo huo.Kulia nimkandarasi wa Mwalo huo Kayumba Tolokoko.
 Kinana akisalimiana na wananchi wa Kata mpya ya Kapalamsenga, Mpanda Vijijini leo.
 Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Kapalamsenga, Wilaya ya Mpanda Vijijini, ambapo alilani kitendo cha Mbunge wa Chadema, Tundu Lisu kumkejeli katika Bunge la Kataiba kuwa alikuwa ni muongo.
 Wananchi wa Kijiji cha nyagala, wilaya ya Mpanda Vijijini, wakitoa maombi yao kwa Katibu Mkuu wa CCM, Kinana la kujengewa Zahanati, baada ya kuuzuia msafara wake uliokuwa ukitokea Kapalamsenga wilayani humo. Kinana aliahidi kusaidiana na serikali kujenga zahanati hiyo.
 Kinana akizungumza na wananchi wa Kijijicha cha Mnyagala na kuahidi kuwa Serikali itasaidia katika ujenzi wa zahanati hiyo.
Kinana akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ikakaka waliosimamisha msafara wa Kinana na kuomba wasaidiwe ujenzi wa shule na visima vima vya maji. Kinana aliwasimamisha  Mkurugenzi wa halmashauri ya Mpanda na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, waeleze watakavyo tekeleza miradi hiyo ya wananchi.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*