KINANA AINGILIA KATI MGOGORO SUGU WA ARDHI KATI YA WANANCHI NA MWENKEZAJI WILAYANI SUMBAWANGA MKOANI RUKWA
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana ameingilia kati Mgogoro wa ardhi
uliokuwa ukifukuta kwa muda mrefu katika kijiji cha Mawenzusi,wilaya ya
Sumbawanga mjini.Mgogoro huo uliohusu Wananchi na anayedaiwa kuwa
Mwekezaji inaelezwa kuwa maamuzi yalikwishatolewa na Mh.Rais Jakaya
Kikwete,kuwa Wananchi wapewe kipao mbele na Mwekezaji apewe kiasi,lakini
mpaka sasa hakuna lililotekelezwa kufuatia Watendaji waliokuwa wamepewa
dhamana ya kulisimamia jambo hilo kusua sua na hatimaye kutopatiwa
ufumbuzi wa haraka.
Kinana yuko mkoani humo kwa ziara ya siku sita ya kuangalia uhai chama,miradi na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi
Comments