KINANA KUFUNGA KAZI MKUTANO WA MWISHO SUMBAWANGA LEO

NA BASHIR NKOROMO
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, anahitisha leo ziara yake katika mkoa wa Rukwa kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika kwenye Viwanja vya michezo vya mjini hapa.

Mkutano huo utakaofanyika kuanzia mida ya tisa alasiri, unatarajiwa kuhudhuriwa na waelfu ya watu, kufuatia mazungumzo ya hapa na pale ambayo yamekuwa yakisika kutoka kwa watu wa rika mbalimbali katika kona na vijiwe kadhaa vya hapa, tangu jana jioni.

Kabla ya kufanya mkutano huo, Kinana atakutana na kuwa na kikao cha ndani na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya mkoa ili kufanya tathmini ya ziara hiyo.

Akiwa mkoani Rukwa ambako aliwasili Machi 30, 2014, Kinana ametembea katika wilaya za mkoa huu zikiwemo, Nkasi, Kalambo na Sumbawanga Vijijini ambako alifanya shughuli mbalimbali ikiwemo mikutano ya hadhara na kukagua shughuli za ujasiriamali katika nyanja kadhaa na utekelezaji wa ilani ya CCM

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI