Marekani imeonyesha wasiwasi wake
kuhusu kile ilichokitaja kama harakati za kundi fulani linalotaka
kujitenga ambalo limekuwa likisaidiwa na Urusi kuchochea ghasia
mashariki mwa Ukrain.
Kufuatia kutekwanyara kwa vituo vya
polisi katika miji kadhaa ya mashariki mwa Ukrain ,waziri wa maswala ya
kigeni nchini marekani John Kerry amesema kuwa mashambulizi hayo ya watu
waliojihami na silaha za Urusi yalifanyika kwa mpangilio.
Katika mazungumzo yao ya simu na
waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov,Kerry ameitaka
Urusi kusitisha mashambulizi kama hayo la sivyo ikabiliwe na vikwazo
zaidi.
Urusi imeonya kuwa utumiaji wowote wa
nguvu nchini Ukrain utahujumu harakati za kidiplomasia kumaliza mgogoro
huo.kwa hisani ya BBC(Awadh Ibrahim) MJENGWABLOG.
Comments