Pazia la ligi kuu Tanzania bara limefungwa rasmi hii leo kwa
timu zote 14 kushuka dimbani , huku miamba miwili ya soka Tanzania,
Yanga na Simba wakitoka sare ya goli moja moja.
Simba ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kipindi cha pili
cha mchezo, likifungwa kiustadi kabisa na Harun Athuman Chanongo na
baada ya dakika takribani tano mbele, Yanga iliweza kusawazisha kupitia
winga wake wa pembeni Simon Msuba kupitia pande alilopigiwa na Didier
Kavumbagu na mchezo kumaliza kwa sare ya bao moja kwa moja na yanga
kuweza kukabidhiwa kombe lake la mshindi wa pili.
Mbali na mchezo huo, kituko kikubwa kilichotokea leo katika
uwanja wa Taifa, ilikuwa ni katika lango la timu ya Simba kulikuwa na
taulo ambalo mlinda mlango wa Simba ‘Ivo Mapunda’ alilokuwa anajifutia
mara zote wakati anataka kudaka mipira akiwa
amelitundika katika nyavu, kitendo kilichotokea kumkera mchezaji mmoja
wa Yanga na kulichukua kisha kulirusha upande wa mashabiki na
kushangiliwa sana.
Lakini kocha wa Simba ‘Zdravko Logarusic‘
alionekana kutopendezwa na tukio hilo na kuamua kumpa mchezaji wa
akiba taulo lake akalipeleka tena langoni kwa timu wa Simba kabla ya
baadae kuja shabiki wa Yanga na kulichukua kisha kutokomea nalo sehemu
isiyojulikana.
Comments