Keki
Maalum iliyoandikwa kumpongeza Bi Asha, ambayo imeandaliwa na baadhi ya
Wajumbe Wanawake wa Bunge Maalum la Katiba kumpongeza Mjumbe wa Bunge
hilo Mh. Asha Bakari Makame kwa umahiri wake wa kupinga udhalilishaji wa
kijinsia ndani ya Bunge hilo na kuwa na msimamo.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Asha Bakari Makame akikata Keki Maalum
kuashiria uzinduzi wa hafla fupi ya kupongezwa kwake kutokana na msimamo
wake ndani ya Bunge Maalum la Katiba linaloendelea Mjini Dodoma. Kushoto kwake ni Waziri wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Maendeleo ya Vijana wanawake na Watoto Mh. Zainab Omar Mohammed.
Comments