msanii wa orijino komedi mpoki aalikwa ujerumani kuhudhuria sherehe za muungano



Msanii maarufu nchini Tanzania  Kutoka kundi la Orijino Komedi al maarufu kama Mpoki a k a Muarabu wa Dubai anatarajiwa kuondoka nchini mapema mwanzo wa wiki hii kwenda nchini Ujerumani kuhudhuria  Mkutano mkuu wa Umoja wa Watanzania Ujerumani (U T U), utakaoambatana na Kongamano la kibiashara pamoja na Sherehe za Muungano wa Tanzania , zitakazoanza  siku ya ijumaa tarehe 25.04.14 na kumalizika siku ya Jumamosi Tarehe 26.04.14.

Mpoki amesema kuwa  umuhimu mkubwa wa safari yake ni  kuwakilisha wasanii wa Tanzania katika Tamasha hili kubwa  la aina yake, na  kufafanua  kuwa wakati umefika kwa wasanii wa Tanzania kushirikiana kikamilifu na Watanzania wanaoishi nje ya nchi ili kuweza kupata fursa mbali mbali  zilizopo huko. 
Amesema  amevutiwa sana na Umoja Wa Watanzania Ujerumani (U T U) kwa shughuli zake   mbali mbali ambazo umekwishazifanya nchini humo  na ameamua kutoa mchango wake wa hali na mali kuhakikisha     (U T U) inafanya vizuri zaidi  na kwamba yeye binafsi amekuwa ni mfuatiliaji wa karibu sana  wa shughuli za umoja huo.

 Mwenyekiti  wa Umoja Wa Watanzania Ujerumani Bw. Mfundo Peter Mfundo alithibitisha  safari ya msanii huyo Maarufu nchini Tanzania, na kusema U T U Ilipendelea sana wasanii zaidi kuhudhuria sherehe hizi lakini kwa bahati mbaya  haikuwezekana  kutokana na mambo yalio nje ya uwezo wao ingawa UTU  ni chombo kinachokubali sana na kuzifagilia kazi za wasanii wa Tanzania.

U T U inamtakia Bw Mpoki Safari njema.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI