PICHA NA VIDEO: SKYLIGHT BAND WAFANYA UZINDUZI RASMI WA NYIMBO YAO MPYA YA KARIAKOO PAMOJA NA KUTAMBULISHA STUDIO YAO MPYA YA KUREKODIA MUZIKI.
Meneja
wa Band ya Skylight Aneth Kushaba akielezea kwa kina uzinduzi Rasmi wa
wimbo wao Mpya unaokwenda kwa jina la Kariakoo ambapo uzinduzi huo
uliambatana na Video pamoja na Audio. Pia ametambulisha Rasmi Studio ya
kurekodi Muziki ambapo sasa nyimbo zao watakuwa wanafanyia katika Studio
yao.
Kutoka
kushoto ni mmoja wa waimbaji wa Skylight Band Sam Mapenzi, (katikati)
ni Meneja wa Band hiyo Aneth Kushaba pamoja na Mwimbaji mwengine wa
Skylight Band Joniko Flower wakiwa wanazungumza na waandishi wa Habari
na wadau mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa wimbo wao mpya wa Kariakoo
pamoja na Kutambulisha Rasmi Studio yao.
Meneja
wa Skylight Band Aneth Kushaba, akitangaza rasmi ratiba zao za show ya
Pasaka ambapo Tarehe 20/04/2014 watakuwa wanashow ya nguvu Mwanza
Skylight Beach Resort (Jembe Beach) ambapo Watakao kata tiketi kabla
itakuwa ni Tsh 10,000 na watakao katia Getini itakuwa ni Tsh 15,000 Pia
tarehe 27/04/2014 kutakuwa na Tamasha maalum la kutambulisha Nyimbo mpya
na wanamuziki wapya Escape One ambapo panafanyika Show za kila Jumapili
,aliongeza kuwa kila siku ya Ijumaa Show huwa Thai Village Masaki.
Comments