TBL YAKABIDHI KISIMA CHA MAJI ZAHANATI YA MVUTI DAR

 Mkuu wa Mahusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Stephen Kilindo (kulia) na Afisa Uhusiano wa Kampuni hiyo, Bi. Doris Malulu, wakimuongoza Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (wa pili kushoto), kwenda kuzindua rasmi mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, Kata ya Msongola, Wilayani Ilala, Dar es Salaam jana, uliojengwa na TBL. (Na Mpigapicha Wetu)
 Kwesi (mwenye suti), akimshika mkono wa pongezi Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Doris Malulu (wa pili kulia), wakati wakielekea kuzindua mradi wa maji katika zahanati ya Mvuti, iliyoko Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, ulichojengwa na TBL. Kulia ni Mkuu wa mahusiano na sheria wa Kampuni hiyo, Bw. Stephen Kilindo.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti), akikata utepe kuzindua rasmi mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, Kata ya Msongola, Wilayani Ilala, Dar es Salaam jana, uliojengwa na Kampuni Bia Tanzania (TBL). Wa pili kulia ni Mkuu wa mahusiano na sheria wa Kampuni hiyo, Bw. Stephen Kilindo, Diwani wa Kata hiyo, Bi. Angelina Malembeka na Ofisa Mauzo wa TBL Ilala, Bw. Godrack Kalebi. (Na Mpigapicha Wetu)

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti kulia), akiondoa kitambaa kuzindua mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, uliojengwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), anayemsaidia ni Ofisa Mauzo wa TBL Ilala, Bw. Godrack Kalebi. Wanaoshudia ni Mkuu wa Mahusiano wa TBL, Bw. Stephen Kilindo na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Dkt. Asenga Severin.  (Na Mpigapicha Wetu)
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti), akijaribu kufungua koki ya bomba la maji, baada ya kuzindua mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, iliyoko Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, kilichojengwa na Kampuni Bia Tanzania (TBL). Wa pili kulia ni Mkuu wa mahusiano na sheria wa Kampuni hiyo, Bw. Stephen Kilindo, Ofisa Mauzo wa TBL,  Ilala, Bw. Godrack Kalebi na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Bi. Doris Malulu. (Na Mpigapicha Wetu)
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti), akisaidia kumtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Mvuti, Bi. Aghata Senga, baada ya kuzindua mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, iliyoko Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, uliojengwa na Kampuni Bia Tanzania (TBL). kulia ni Mkuu wa Mahusiano na sheria wa TBL, Bw. Stephen Kilindo, Ofisa Mauzo wa TBL kanda ya Ilala, Bw. Godrack Kalebi (wa pili kulia) na Diwani wa Kata hiyo, Bi. Angelina Malembeka (mwenye kilemba kushoto).

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA