Kampuni
kubwa ya uundaji na uuzaji wa magari ya Japan, Toyota i meagiza magari
milioni sita unusu kurejeshwa ilikufanyiwa ukarabati kutokana na
upungufu mbalimbali.
Idadi hiyo ya kurejeshwa magari ni kubwa mno kurejeshwa viwandani.
Kampuni hiyo kubwa zaidi duniani ya uundaji magari inarejesha magari aina ya Yaris, Urban Cruiser, RAV4 na Hilux.
Kuna
hitilafu katika kifuko cha hewa cha kumlinda dereva -(air bag) katika
jumla ya magari milioni tatu, ikiwa haiwezi kuchomoka ili kimlinda
dereva wakati wa ajali.
Aidha kuna hitilafu pia katika baadhi ya viti, usukani na kifaa cha mota ya kuwasha magari.
Kampuni
ya Toyota inasema haijabaini ni ajali ngapi, majeruhi au maafa ambayo
yamesababishwa na matatizo hayo yaliyogundulika majuzi.
Jumla ya magari 20,000 yanahitilafu ya mota ya kuwasha.
Mwezi
Februari, Toyota iliagiza magari milioni 1.9 aina ya Prius hybrid
yaregeshwe kutokana na hitlafu iliyopelekea magari hayo kupoteza mwendo
ghafla.
Kwa Jumla magari milioni 25 yamearegeshwa katika kipindi cha miaka miwili u nusu iliyopita.Chanzo BBC Swahili
Comments