Bendi
ya African Stars “Twanga Pepeta” itasindikiza uzinduzi wa Redds Miss
Tabata itakayofanyika Jumapili ya Pasaka katika ukumbi wa Da’ West Park,
Tabata.
Mratibu
wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema bendi hiyo itatambulisha nyimbo
zao mpya kama zawadi yao ya Pasaka kwa wapenzi wao.
Pia bendi hiyo ijulikanayo kama Wakali wa Kisigino pia watapiga nyimbo zao zote kali hadi majogoo.
Mratibu
huyo wa Bob Entertainment na Keen Arts alisema kuwa wapenzi wa urembo
watapata fursa ya kuwaona warembo hao siku hiyo kabla hawajashiriki
kwenye shindano la Miss Tabata ambalo limepangwa kufanyika mwishoni mwa
mwezi ujao.
Katika uzinduzi huo warembo wa Tabata watasindikizwa na washiriki wenzao wa Miss Mzizima na Miss Ukonga.
Pia
watakuwepo viongozi waandamizi kutoka kamati ya Miss Tanzania
ikiongozwa na Hashim Lundenga na Redds Miss Tanzania Happiness
Watimanywa.
Warembo
21 wanaendelea na mazoezi ya Miss Tabata katika ukumbi wa Da West Park
chini ya wakufunzi wawili - Neema Chaki na Pasilida Bandari.
Warembo
hao ni Esther Frank Kiwambo (20), Jemima Huruma Mawole (22), Badra S.
Karuta (20), Mercy Mathias Kazula (19), Lydia Charles (22), Agnes Tarimo
(18), Agnes Alex (20), Catrina Lawrence Idfonsi (20), Nuru Omary
Athumani (19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).
Wengine
ni Annatolia Raphael (21), Mary Henry (21), Evodia Peter (22), Fatma
Hussein Ismail (20), Ester Wilson Mbayi (20), Ambasia Lucy Mally (22),
Faudhia Hamisi (21), Najma Charles Mareges (19), Lightnes Olomi (18),
Husna Ibrahim (19) na Ramta Mkadara (20).
Warembo watano kutoka Tabata watashiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Dorice Mollel ambaye pia ni Redds Miss Ilala.
Comments