Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi, Alex Msama akizungumza na baadhi ya Wanahabari
kwenye moja ya mikutano yake kuhusiana na tamasha la pasaka.
KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, mwishoni mwa wiki ilitangaza viingilio vya tamasha hilo jijini Dar es Salaam, viti vya kawaida ni shilingi 5000 na watoto 2000. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Alex Msama viti maalum ni shilingi 20,000 wakati VIP ni shilingi 10,000.
Msama
alisema hivi sasa wanaendelea na mchakato wa kufanikisha zoezi la mgeni
rasmi katika tamasha hilo kwani hivi karibuni watakamilisha zoezi la
upigaji kura kumchagua.
Msama alisema mchakato wa kuelekea katika tamasha hilo litakalofanyika jijini Dar es Salaam Aprili 20 na baadaye mikoa mingine saba hapa nchini.
Aidha
Msama alitoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam kujiandaa na tamasha hilo
ipasavyo kwani lina mlengo wa kurudisha mapato yanayopatikana na
kuyapeleka katika maeneo matatu ambayo yanawahusu, yatima, walemavu na
wajane.
Msama
alisema mipangilio yake ya kuwawezesha wenye uhitaji maalum ni
kuwajengea kituo kitakachokuwa katika eneo la Pugu nje kidogo ya jiji la
Dar es Salaam ambacho kitajulikana kama Jakaya Mrisho Kikwete, rafiki
wa wasiojiweza.
Comments