Wananchi waaswa kuachana na Matumizi ya Vipimo visivyo Rasmi

 Kaimu Meneja Sehemu ya Habari toka Wakala wa Vipimo Bi. Irene John akiwaeleza jambo waandishi wa Habari (hawapo pichani) na kuwatahadharisha wananchi kuhusu matumizi ya vipimo batili unaofanywa kwa kusutumia visado na ndoo za Plastiki. Wanaofuata Kushoto kwake ni Afisa Habari Idara ya Habari (MAELEZO) Frank Mvungi,Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi Bw. Peter Masinga na Mwisho ni Meneja wa Upimaji Bw. Richard Kadeghe.
 Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano wa Wakala wa Vipimo leo Jijini Dar es Salaam.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.
 Mkuu wa Kitengo cha Sheria Toka Wakala wa Vipimo Bw. Moses Mbunda akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mchakato wa Kunazisha Sheria Mpya itakayosaidia kuimarisha Sekta ya Upimaji Nchini, Kulia ni Kaimu Meneja Sehemu ya Habari toka Wakala wa Vipimo Bi. Irene John. 
Meneje wa Upimaji toka Wakala wa Vipimo Bw. Richard Kadeghe akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ambavyo vipimo batili vinayotumika.

=========  =======  ========
Na Frank Mvungi MAELEZO.

Serikali yawatahadharisha wananchi kuhusu matumizi ya vipimo batili hususani visado na ndoo za Plastiki.

Hayo yamesema na Kaimu Meneja wa  Habari,Elimu na Mawasiliano  wa EWakala wa Vipimo Tanzania Bi Irene John wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Akieleza Bi Irene amesema ufungashaji na upimaji batili ni kinyume cha sheria ya Vipimo sura 340 (iliyopitiwa mwaka 2002) pamoja na Kanuni zake.

Akifafanua zaidi  alisema ufungashaji na matumizi ya vipimo batili hudhoofisha uchumi wa Taifa kwa kuwa humpunja mkulima,mlaji,mfanyabiashara na mtumiaji.

Aliongeza kuwa Serikali imekuwa ikipoteza mapato yake ambapo Halmashauri hukusanya mapato pungufu wanapotoza ada kwa gunia badala ya uzito au ujazo.

Irene  alitaja athari nyingine kuwa ni kuathiriwa kwa biashara ya kimataifa kutokana na wananchi kutokuzingatia vipimo hasa kwa kutumia mizani wakati wanapofanya biashara ya kununua na kuuza.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya ufundi wa wakala huo bw.Peter Masinga alisema ni vyema wananchi wakaacha kutumia vipimo batili kwani vimekuwa vikidhoofisha ukuaji wa uchumi kwa muda mrefu na hivyo kwenda kinyume na jitihada za Serikali za kuwaletea maendeleo wananchi.

Bw. Peter aliongeza kuwa kuanzishwa kwa vituo vya kununulia mazao vijijini ni moja ya hatua zitakazosaidia kuondoa tatizo la vipimo batili kwa kuwa Serikali itaweza kusimamia kwa ukaribu matumizi ya vipimo sahihi kama vile mizani.

Wakala wa vipimo ni Wakala wa Serikali ambayo ilianzishwa Mei,2002 kwa Tangazo la Serikali namba 194 kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi, jukumu kuu likiwa kumlinda mtumiaji kupitia matumizi ya vipimo sahihi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.