WANAWAKE NGORONGORO WAUNDA BARAZA LA KUSAIDIA MTOTO WA KIKE

Kutokana na kukithiri kwa mfumo dume unaoambatana na ukandamizaji wa mwanamke na kusababisha ongezeko la watoto yatima na wajane katika jamii ya wafuagaji wa kimasai, wanawake wa jamii  hiyo wanaoishi ndani  ya eneo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wameunda baraza  la wanawake  litakalosimamia masuala mbalimbali kwa mtoto wa kike husani elimu,afya,na haki ya mwanamke.

Wanawake hao wa jamii ya kimasai wanabainisha kuwa hamasa ndogo ya jamii ya kuwasomesha watotot wa kilke na kutopewa kipaumbele ,afya duni ya jamii hasa mama na motto endapo vitazingatiwa katika jamii hiyo vitasaidia kuondokana na changamoto hizo na hatimae kuongeza idadi ya wasomi hasa watoto wa kike ambao wataikomboa jamii hiyo kwa ujumla .

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza hilo  uliofanyika katika makao makuu ya mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro ukienda sambamba na harambee ya kuchangia mfuko wa elimu kwa watoto wa kike  makamu mwenyekiti wa baraza hilo bibi mereyo muresi anasema   litakua chombo muhimu cha kuwasemea wanawake katika vyombo vya maamuzi ndani na nje.

Mhifadhi mkuu wa mamlaka ya ngorongoro  dakta  fredy manongi ndiye aliyezindua baraza hilo na kuendesha harambee iliyofanikisha kupatikana kwa zaidi ya shilingi milioni sabini fedha taslimu na ahadi.

Baraza la wanawake  hao wafugaji linaanzishwa huku tayari kukiwa na baraza la wafugaji ngorongoro ambalo mwenyekiti wa baraza hilo metui ole shaudo anawaasa  kuwa lengo walilokusudia  la kumkomboa mwanamke litafikiwa kwa  wao kushirikiana na wadau wengine

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU