m Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi amesema anawaheshimu na kuwakubali wanaCCM wa Pemba kwa misimamo yao thabiti katika kuilinda na kuitetea CCM, bila kuyumba. Dkt. Nchimbi pia amewapongeza kwa jinsi ambavyo wameendelea kuwa imara kuifanya Pemba kuwa mojawapo ya ngome za Chama Cha Mapinduzi nchini, akiwasisitiza wanaCCM kuendelea kuwa wamoja, chini ya Uongozi wa Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. SAMIA Suluhu Hassan. Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi amesema hayo leo Jumamosi, Machi 23, 2024, alipokuwa akizungumza na baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM wa Pemba, waliofika kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume, Pemba, mara tu baada ya kuwasili uwanjani hapo, tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku moja, katika Kisiwa cha Pemba. “Kati ya wanaCCM ninaowaheshimu na kuwakubali sana kwa jinsi wanavyoipenda CCM, wanavyoilinda, kuitetea na kuisemea ni wanaCCM wa Pemba. Asanteni sana k
Comments