ABOUBAKAR SADIK APASULIWA



 

Stori: Joseph Shaluwa

AFYA ya mtangazaji mwenye jina kubwa Bongo, Aboubakar Sadik ambaye anatumikia Radio One Sterio ya jijini Dar es Salaam, si nzuri kiasi cha kulazimika kufanyiwa upasuaji haraka.

Mtangazaji  wa Radio One Sterio mwenye jina kubwa Bongo, Aboubakar Sadik akifanyiwa upasuaji.
Habari kutoka chanzo chetu cha kuaminika, zinasema kuwa, Abou alizidiwa ghafla Jumamosi ya Julai 26, mwaka huu akiwa kazini kwake na kukimbizwa katika Hospitali ya Hindu Mandal, Posta jijini Dar es Salaam.
“Alikuwa mzima kabisa, alizidiwa ghafla na kukimbizwa Hindu Mandal ambapo alifanyiwa upasuaji,” kilisema chanzo chetu.

Risasi Mchanganyiko lilipotaka kujua aina ya upasuaji aliofanyiwa Abou, chanzo kikafunguka: “Ndugu yangu, suala la ugonjwa ni siri ya mgonjwa na daktari wake, labda uwasiliane naye, maana ametoka hospitali leo asubuhi (Jumatatu), ana nafuu nzuri.”
Aboubakar Sadik akiwa Hospitali ya Hindu Mandal, Posta jijini Dar es Salaam.
Baadaye mchana chanzo hicho kilimtumia picha mbalimbali za Abou akiwa hospitalini hapo, ikiwemo aliyokuwa chumba cha upasuaji wakati shughuli ikiendelea.
Mwandishi wetu alipomtafuta mtangazaji huyo kupitia simu yake ya mkononi, hakupokea hivyo akalazimika kumtumia ujumbe uliosomeka: “Pole kaka, nimepata taarifa unaumwa. Nini zaidi? Unaendeleaje sasa?”
Muda mfupi kabla ya kuelekea mitamboni, Abou alijibu: “Shukrani kaka. Ni kweli, nilifanyia surgery (upasuaji) Hindu Mandal, lakini nimesharuhusiwa, nashukuru Mungu ilikwenda vizuri.”
Abou anawika na vipindi mbalimbali Radio One vikiwemo Nani Zaidi, Chombeza Time, Mtaa wa Mangoma na Flavor 120.Chanzo GPL

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU