Al-Shabaab washambulia ikulu Somalia



Ikulu ya Rais iliwahi pia kushambuliwa mwezi Februari
Vikosi vya serikali Somalia vimefanikiwa kuidhibiti upya ikulu ya rais katika mji mkuu Mogadishu baada ya wapiganaji wa Al Shabaab kuishambulia.


Maafisa wanasema washambuliaji wapatao watano kutoka kundi la al-Shabab - waliuawa walipoingia katika eneo la ikulu hiyo.
Washambuliaji hao wanadaiwa kulipua bomu lililotegwa kwenye gari karibu na langu kuu la Ikulu hiyo.

Waziri wa habari wa Somalia Mustaf Dhuhulow
Waziri wa habari na mawasiliano wa Somalia Mustaf Dhuhulow ameambia BBC kuwa tayari mmoja wa washambuliaji hao amekamatwa na anahojiwa na polisi.
Waziri Mustaf amesema, '' Walishambulia ikulu ya rais saa za jioni. Alikuwa watu washambuliaji watatu pamoja na dereva wao.
Washambuliaji hao waliuawa lakini dereva wao alipata majeraha madogo na anazuiliwa na polisi na kuhojiwa.
Walijaribu kuvamia Villa Somalia lakini wakakomeshwa. Tutawapa maelezo zaidi baadaye. Na tutaweza kutoa maelezo zaidi kwa raia wa Somalia na dunia nzima.''

Shambulio la Al shabaab Mogadishu
Hii ni mara ya pili kwa Al Shabaab kuvamia ikulu ya rais mjini Mogadishu mwaka huu japo mara ya kwanza walifanikiwa kuingia ndani.
Rais Hassan Sheikh Mohamoud hakuwepo wakati wa shambulio hilo.
Kundi la wapiganaji wa kiislamu Al shabaab limefukuzwa kutoka mjini Mogadishu tangu mwaka wa 2011 lakini limekuwa likifanya mashambulio ya kuvizia tangu wakati huo.


Wanamgambo hao wanaaminiwa kufanya mashambulio kadhaa pia katika nchi jirani ya Somalia kama vile Kenya, Uganda na Tanzania kama njia ya kulipiza kisasi kwa kuingia majeshi ya Umoja wa Afrika nchini Somalia.Chanzo BBC Swahili

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*