ASERNAL, CHELSEA ZAFANYIANA UMAFIA USAJILI WA SAMI KHEDIRA, WAKALA AMWAGA MCHELE KWEUPE!



On the move: Sami Khedira has not signed a new deal at Real Madrid and is set to leave
Anatimka: Sami Khedira hajasaini mkataba na klabu yake ya Real Madrid na yuko mbioni kuondoka.
 
KLABU ya Chelsea imepata nguvu ya kupambana kumsajili Sami Khedira baada ya jumatano usiku wakala wa mchezaji huyo kusema hakuna dili lolote lililokamilika na Asernal.
Kocha wa Blues, Jose Mourinho alimsajili beki wa kushoto  Filipe Luis jana kutokea klabu ya Atletico Madrid kwa dau la paundi milioni 18 na sasa ametua nyavu zake kwa Mjerumani Khedira.
Ilifahamika kuwa Arsenal wamekubaliana ada ya uhamisho ya paundi milioni 20 na Real Madrid ili kuinasa saini ya nyota huyo mwenye miaka 27, lakini walikuwa wanahangaikia suala la mshahara ambapo mchezaji huyo anahitaji paundi laki moja na elfu themanini kwa wiki.
Hata hivyo, wakala wa  Khedira, Jorg Neubauer alisema: "Hatuko kwenye mazungumzo na Arsenal. Sidhani kama makubaliano ya ada yanaweza kufanyika, vinginevyo ningekuwa nimeambiwa."
"Khedira anapendwa na Mourinho tangu wakati huo yupo Real Madrid na kocha huyo anaeleweka hivyo. Hilo pia limehamia akiwa Chelsea".
Khedira yupo tu kutokana na wawakilishi wa Real Madrid na mchezaji kushindwa kufikia makubaliano ya kuongeza mktaba.
Neubauer aliongeza: "Tupo katika mzungumzo na Real Madrid kuhusu mkataba, lakini hakuna kinachokaribia kuamuliwa. Sami amerudi kutoka kombe la dunia na amekwenda likizo".
World Cup winner: The German has been linked with a move to Arsenal and Chelsea
Mshindi wa kombe la dunia: Mjerumani huyu anahusishwa kujiunga na klabu za Chelsea na Asernal 
Recruit: Chelsea boss Jose Mourinho has already acquired Diego Costa and Filipe Luis
Anasuka kikosi: Bosi wa Chelsea, Jose Mourinho tayari ameshainasa saini ya Diego Costa na Filipe Luis

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI