CHIKAWE AMWAGA MISAADA YA MABATI 100 NA JEZI ZA MIPIRA NACHINGWEA

       

PIX  1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kulia), akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Nditi, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo ya Nditi wakati alipofanya ziara katika kata hiyo iliyopo Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe alitoa mabati 100 kwa ajili ya ujenzi ya Ofisi Kuu ya CCM katika Kata hiyo ya Nditi. Picha na Felix Mwagara.
PIX 2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kulia), akimkabidhi jezi za timu sita za mpira wa miguu Afisa Mtendaji wa Kata ya Nditi, Patrick Mwasambungu kwa ajili ya kuzikabidhi timu hizo zilizopo katika Kata hiyo katika Jimbo la Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe pia alitoa mabati 100 kwa ajili ya ujenzi ya Ofisi Kuu ya CCM katika Kata hiyo ya Nditi. Mbunge huyo wa Nachingwea yupo jimboni mwake kwa ajili ya kufanya ziara ya kuzungumza na viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali. Picha na Felix Mwagara.
PIX 3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kushoto), akikiangalia kifusi cha mchanga kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mnerongongo ambayo ipo katika hatua ya mwisho kukamilika ujenzi wake. Katika ujenzi wa ofisi hiyo, Waziri Chikawe alitoa mabati 100 ambayo tayari yameezekwa. Mbunge huyo wa Nachingwea yupo jimboni mwake kwa ajili ya kufanya ziara ya kuzungumza na viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali. Picha na Felix Mwagara.
PIX 4
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kushoto), akikagua ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mnerongongo ambayo ipo katika hatua ya mwisho kukamilika ujenzi wake. Katika ujenzi wa ofisi hiyo, Waziri Chikawe alitoa mabati 100 ambayo tayari yameezekwa. Mbunge huyo wa Nachingwea yupo jimboni akifanya ziara ya kuzungumza na viongozi wa CCM katika Kata za Wilaya za Nachingwea mkoani Lindi. Picha zote na Felix Mwagara.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA