DIAMOND AMVISHA TENA PETE YA UCHUMBA WEMA SEPETU

Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu (25) akionyesha pete aliyovishwa na Diamond.

Wema Isaac Sepetu (25) ameibua viulizo baada ya kuonekana akirandaranda na pete ya ndoa kidoleni ikidaiwa kuwa amevalishwa na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa siri kubwa,Baada ya kuwepo kwa habari nyingi kuhusiana na ishu hiyo, Ijumaa Wikienda liliingia mzigoni kusaka ukweli wa ishu hiyo na kujua mbivu na mbichi.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa mkali huyo wa sinema za Kibongo, hata mashosti zake hawajui kinachoendelea zaidi ya kuulizana wao kwa wao kuhusu nini kinaendelea huku kukiwa na hisia kuwa huenda wawili hao wamefunga ndoa ya siri.



Muonekano wa karibu zaidi wa pete hiyo katika kidole cha Wema.

 ALISHAMVISHA YA UCHUMBA
Kuna maelezo kwamba Diamond alifanya hivyo ili kuzuia mwanaume mwingine kumvisha Wema pete ya ndoa kwani alishamvisha ya uchumba tangu mwaka 2011 kwenye Ukumbi wa New Maisha ulipo Masaki jijini Dar.
WEMA LAIVU
Wiki iliyopita jitihada za kumnasa Wema akiwa na pete ya uchumba zilizaa matunda ambapo mwanahabari wetu alimuweka ‘mtukati.
Wema alipotakiwa kuanika ukweli juu ya pete hiyo, alikubali na kueleza kuwa ameamua kufunguka kwa mwanahabari wetu baada ya kuwa kimya tangu alipovishwa pete hiyo.

Wema Isaac Sepetu akiwa na mpenzi wake Diamond.

 HAJAFUNGA NDOA LAKINI…
Wema alisema si kweli kwamba amefunga ndoa ya siri ila Diamond alimvisha pete hiyo kama urembo akijua kabisa kwamba yeye ni wife material (anafaa kuwa mke).
“Sijafunga ndoa jamani. Hii pete alininunulia baby wangu Nasibu (Diamond) wakati tukiwa South Africa (Afrika Kusini). 
WEMA AIONA PETE, YAMVUTIA

“Alininunulia na kunivisha tulipokwenda kwenye Tuzo za MTV Africa (MAMA). Nakumbuka tuliingia kwenye duka moja nikaiona hii pete ikanivutia sana, nikamwambia Nasibu ndipo akaninunulia na kunivisha palepale.
Wema Isaac Sepetu akiwa na mkwewe, mama Diamond.

 “Cha kushangaza ni kwamba imewatatiza wengi na kuhisi ndoa tayari.
“Hii pete ndogo niliinunua mwenyewe  hapahapa Bongo na kuivaa kama urembo tu, hakuna tofauti na hilo kuhusiana na hizi pete nilizovaa kidole husika,” alisema Wema ambaye kidoleni kwake kunaonekana pete mbili, kubwa na ndogo. 
WEMA NI WIFE MATERIAL?
lipoulizwa kwa nini Diamond aliamua kumvisha pete hiyo kabla ya ndoa, Wema alifunguka: “(kicheko) hilo sina uhakika nalo but amegundua mimi ni wife material hataki kunipoteza. Kanipa heshima anayostahili kupewa mwanamke...” 
AMSHUKURU MTABIRI

Wakati huohuo, Wema amemshukuru mtabiri, Maalim Hassan Yahya ambaye mwanzoni mwa mwaka huu alitabiri kuwa mastaa hao wataoana mwezi ujao (Agosti) mwaka huu akiomba Mungu na iwe hivyo.
“Natamani hiyo ndoa na nasubiria hiyo siku ili utabiri utimie, ni jambo la heri jamani,” alisema Wema. 
DIAMOND VIPI?
Alipotafutwa Diamond ili afunguke kuhusiana na ishu hiyo, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa. Wakati huohuo, mashabiki wa mastaa hao, wamewashauri mama Wema na mama Diamond kuwa kitu kimoja ili kufanikisha ndoa hiyo ya watoto wao. 
NI PETE YA PILI YA NDOA!
Ukiacha pete hiyo ya ndoa aliyovishwa na Diamond, Wema aliwahi kuvishwa pete kama hiyo alipofunga ndoa na jamaa aitwaye Jumbe Yusuf Jumbe ambayo haikudumu hata mwezi mmoja.KUTOKA KWA MHARIRI
Ijumaa Wikienda linawatakia kila la heri mastaa hao ili kufanikisha jambo hilo ambalo linaongeza heshima kwenye jamii.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU