ISRAEL YAONGEZA MUDA WA KUSITISHA MAPIGANO KWA MASAA 24 ZAIDI UKANDA WA GAZA PALESTINA, ZAIDI YA WATU 1300 WAPOTEZA MAISHA.

http://nofalliata.files.wordpress.com/2012/02/nena_palestina_tanque_israel_revipossiblepart-blogspot-com1.jpg

Mpalestina akibeba vitu vyake alivyopata baada ya nyumba yake kubomolewa huko Beit Hanoun Julai 26, 2014.

Baraza la mawaziri la Israel limekubali ombi la Umoja wa Mataifa kuongeza muda wa kusitisha mapigano kwa saa 24, baada ya muda wa saa 12 kumalizika Jumamosi.

Afisa wa serikali ya Israel amesema, mashambulio yatasitishwa hadi saa sita za usiku Juampili, lakini Israel itajibu shambulio lolote la roketi litakalofanywa na wapiganaji wa Hamas, na kuendelea kutafuta na kuharibu njia za chini kwa chini huko Gaza.

Viongozi wa Hamas wamekata kutambua muda huo uloongezwa wakidai kuondolewa kwanaza wanajeshi wa Israel kutoka Gaza. Wapiganaji wa Hamas walifyetua roketi kadhaa ndani ya Israel mara baada ya muda wa awali wa saa 12 kumalizika Jumamosi lakini majeshi ya Israel hayakujibu.


Mama wa Kipalestina akionesha picha za vijana wake waliouliwa wakati wa mashambulizi ya Israel.
huko Gaza.


Kusitishwa mapigano kwa muda siku ya Jumamosi kuliwapatia wakazi wa Gaza nafasi ya kurudi katika nyumba zao na kutizama kilichobaki kutokana na uharibifu mkubwa wa nyumba na mali ulofanywa na mashambulizi ya Israel.

Idadi ya wa-Palestina walouwawa hadi Jumamosi imepindukia elfu moja na waokozi waliweza kupata miili 100 wakati mapigano yaliposita. Wa-Israeli wamepoteza wanajeshi 37 na raia 2.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI