KANISA LA MORAVIAN LAFANYA MAOMBI KUMALIZA MGOGORO



wachungaji wakifanya maombi maalumu na kukemea katika maeneo yaliyokuwa yameguswa zikiwemo ofisi za Askofu, Lango la kuingilia pamoja na Geti kuu.




 Mchungaji Amos Mwampamba akiendesha ibada hiyo






Mchungaji Watson Mwashambwa akisoma tamko kwa niaba ya waumini na wauchungaji wa kanisa la Moravian





KANISA la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi limeendesha ibada maalumu ya kuliombea kanisa hilo kutokana na vurugu zinazoendelea zikiwemo kufunga ofisi kuu za Jimbo kwa makufuli na minyororo na baadhi ya wachungaji na wakristo Julai 15, mwaka huu.
Awali kabla ya kuanza kwa ibada na mkutano wachungaji hao walifanya maombi maalumu na kukemea katika maeneo yaliyokuwa yameguswa zikiwemo ofisi za Askofu, Lango la kuingilia pamoja na Geti kuu.
Ibada hiyo iliyofanyika jana katika Kanisa kuu la Jimbo hilo lililopo Jakaranda jijini Mbeya iliyoongozwa na Mchungaji Amos Mwampamba na kuhudhuriwa na wachungaji wa Kanisa hilo zaidi ya 100 ilienda sambamba na tamko la kulaani vitendo hivyo.
Akisoma tamko mbele ya wachungaji na waumini kwa niaba ya Wachungaji wa Jimbo, Mchungaji Watson Mwashambwa, alisema kitendo kilichofanywa na wachungaji hao ni kinyume cha utaratibu wa kanisa pia ni matakwa yao binafsi na sio mawazo ya waumini na wachungaji wote.
Alisema kitendo cha waumini wakiongozwa na Mchungaji wa Usharika wa Bethlehemu Edward Chilale kufunga ofisi za jimbo kwa lengo la kumshinikiza Askofu Alinikisa Cheyo ni kutokana na Askofu kuwaonya mara kwa mara kwa vitendo vyao kinyume na kanisa.
Alisema baada ya kuonekana Askofu anawafuatilia sana wakaamua kumuundia zengwe wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jimbo Mchungaji Nosigwe Buya la kutaka ajiuzulu wadhfa wake.
Hata hivyo Wachungaji hao wameitaka Serikali kutoingilia masuala ya Kanisa kwa madai kuwa wanashinikiza kufanya maamuzi kinyume cha katiba na nje ya vikao halali.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mbeya ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Norman Sigalla wakitaka Kanisa hilo kumaliza mgogoro kwa kuitisha mkutano wa Sinodi haraka iwezekanavyo na kumrudisha mwenyekiti madarakani.
Kutokana na kauli hiyo Kanisa hilo limetoa msimamo wa kuendelea kumsimamisha Mwenyekiti wake Nosigwe Buya hadi mwaka 2016 itakapoitishwa Sinodi kwa mujibu wa katiba na kwamba kusimamishwa kwa Mwenyekiti ni kwa mujibu wa Ibara ya 11(2) ya kazi ya Halmashauri kuu xxvi.
Walisema kitendo cha Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya cha kuwaita baadhi ya waumini na kuwakutanisha na Halmashauri kuu kwenye kikao cha usuluhishi ni kuidharau Halmashauri na kupuuza  mamlaka yake kikatiba.
Aidha ibada hiyo ambayo ilikuwa na mkutano ndani yake ni muendelezo wa mgogoro unaofurukuta ndani ya Kanisa hilo Jimbo la Kusini Magharibi unaotokana na kugawanyika kwa wachungaji na waumini kuwa katika pande mbili.
Katika mgogoro huo wapo waumini na baadhi ya wachungaji wanaoshinikiza Askofu Alinikisa Cheyo kujiuzulu na kurudishwa madarakani kwa Mwenyekiti Nosigwe Buya huku kundi lingine likiunga mkono kusimamishwa kwa Mwenyekiti na Askofu kuendelea kuwa madarakani.

Hata hivyo uchunguzi wa Mbeya yetu umebaini kuwa katika ibada hiyo wachungaji waliohuduria niwa upande unaomuunga mkono Askofu Alinikisa Cheyo hali iliyopelekea kutoa matamko ya kukilaani kikundi kinachomuunga mkono Mwenyekiti na kusisitiza kuondolewa madarakani.
Mwisho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.