Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa
Ritta Kabati kulia akikagua choo cha soko la Kitwiru soko ambalo limekimbiwa na
wafanyabiashara baada ya kukosa umeme (picha na Francis Godwin Blog)
Diwani wa kata ya Kitwiru katika Manispaa ya Iringa Ally Mbata wa pili kulia akimwonyesha mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) jiwe la msingi ambalo liliwekwa na kiongozi wa mbio za mwengi Kitaifa mwaka 2012 wakati wa uzinduzi wa soko la Kitwiru ambalo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa halitumiki kutokana na kukosa umeme soko hilo limejengwa kwa zaidi ya Tsh milioni 22 (picha na Francis Godwin Blog)
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) ameanza ziara ya kukagua miradi mbali mbali katika jimbo la Iringa ikiwa ni pamoja na kulitembelea soko lilolozinduliwa na mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2012 ambalo wafanyabiashara wamelihama kutokana na kukosekama kwa huduma ya umeme .

Soko
hilo lililopo eneo la kata ya Kitwiru katika Manispaa ya Iringa
awali lilikuwa likitumiwa vema kabla ya mambo ya siasa kuingizwa kwa
wafanyabiashara kuhamasishwa kuhama eneo hilo na kwenda kufanya
biashara yao eneo la Mashine tatu badala ya kwenda katika soko hilo
la kisasa kwa madani ni porini.
Akiwa
katika ziara hiyo jana sokoni hapo diwani wa kata ya Kitwiru Ally
Mbata alimweleza mbunge Kabati kuwa soko hilo lilijengwa kwa ajili
ya kuwawezesha wafanyabiashara wa kata ya Kitwiru kupata eneo la
kufanyia biashara pia wananchi kupata soko kwa ajili ya kununua
mahitaji mbali mbali.
Hata
hivyo alisema soko hilo ambalo lilifahamika kama gulio la kata ya
Kitwiru lilikuwa likifanay kazi vizuri na uongozi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Iringa uliboresha zaidi kwa kupeleka huduma ya maji na
vyoo vya kisasa ila tatizo lililopelekea wafanyabiashara kuhama ni
umeme kutokana na soko hilo lilikuwa likifanya kazi kila jumapili
kuanzia mchana hadi jioni pekee.
Mbata
alisema ili soko hilo liweze kufikiwa na huduma ya umeme ni nguzo
tatu pekee ndizo zinazohitajika kufikisha umeme katika soko hilo .
Aidha
alisema soko hilo iwapo lingeboreshwa kwa kuwekwa umeme lilikuwa
ni kitega uchimi kikubwa kwa kata hiyo ya Kitwiru japo alisema upo
mkakati wa kulifufua soko hilo.
Kwa
upande wake mbunge Kabati alisema kuwa lengo la ziara yake hiyo
katika soko hilo na maeneo mengine imelinga kuangalia utekelezaji wa
ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) na kuona miradi ambayo inaanzishwa
inaendelezwa kwa kiasi gani .
Alisema
ataendelea kufanya ziara katika miradi mbali mbali ili kuona
usimamizi wa miradi hiyo na ile lenye changamoto kama huo basi
kuangalia uwezekano wa kuiendeleza kwa faida ya wananchi ambao ni
wahitaji wa miradi hiyo ya kimaendeleo .
Mbunge
kabati alisema kuwa soko hilo la Kitwiru iwapo lingeendelezwa
lilikuwa na faida kubwa kwa vijana na wanawake ambao wageweza
kupata ajira zaidi katika soko hilo kwa kufanya biashara mbali mbali
ila kuendelea kubaki pasipo kutumika kwa soko hilo ni hasara kubwa
kwa serikali hasa ukizingatia kiasi kikubwa cha fedha zilizotumika
katika ujenzi wa soko hilo .
MWISHO
Comments