MGOMBEA URAIS WA MSUMBIJI ATUA TANZANIA KUSAKA KURA, AKUTANA NA MAMA MARIA NYERERE KUOMBA BARAKA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimlaki Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi cha FRELIMO, Filipe Nyusi alipowasili leo jioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya ziara ya siku tatu, kusaka kura kwa wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania, kufuatia kampeni za Urais zinazoendelea nchini kwake.

Mgombea huyo wa Urais Filipe Nyusi akimsalimia Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia alifika Uwanja wa Ndege pamoja na Kinana. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.

 Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Filipe Nyusi akisalimiana na wana-CCM waliofika kumlaki Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Kulia ni Mwenyeji wake, Abdulrahman Kinana

 Nyusi akidhihirisha furaha kwa mapokezi aliyopata

 Mgombea huyo wa Urais wa Msumbiji akiwa na Mwenyeji wake, Kinana wakati wa mapokezi yaliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
Filipe Nyusi akizungumza na waandishi wa habari baada ya mapokezi, Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.

 Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mama Maria Nyerere (watatulkushoto) akiwa na ugeni wa mgombea huyo wa Urais nchini Msumbiji, Filipe Nyus (wapili kushoto), nyumbani Mwalimu, Msasani, Dar es Salaam. Kushoto ni Kinana

 Mama Maria Nyerere akimsalimia Mtoto wa Rais wa Kwanza wa Msumbiji Samora Machel, Samora Samora ambaye alifuatana na mgombea huyo wa Urais wa Msumbiji.

 Mama Maria Nyerere akizungumza na mgombea huyo wa Urais wa Msumbiji Filipe Nyus (wapili kushoto) na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana

 Nyusi na Kinana wakimsikiliza kwa makini Mama Maria Nyerere wakati wa mazungumzo hayo

Samora Samora akizungumza na Binti wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, wakati wa ugeni huo nyumbani kwa  Mama Maria Nyerere, Msasani Dar es Salaam. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI