Mtumishi NMB kortini kwa wizi wa Sh1 bilioni

                  

kisutu_7c8f0.gif
Dar es Salaam. Mtumishi wa Benki ya NMB, Mtoro Suleiman na wenzake wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka 13 yakiwamo ya kuiibia benki hiyo zaidi ya Sh1 bilioni na kutakatisha fedha haramu.
Mtoro na wenzake, Daudi Kindamba na John Kikopa walipandishwa kizimbani mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali, Pius Hilla.(E.L).
Imeelezwa kuwa kwa nyakati tofauti, washtakiwa walikula njama, kuiibia benki hiyo kwa njia ya udanganyifu, kutakatisha fedha na kuisababishia hasara ya kiasi hicho cha fedha.
Wakili Hilla alisema kuwa washtakiwa hao walitenda makosa hayo, katika tarehe tofauti kati ya Januari Mosi, 2007 na Julai 30, 2009 katika makao makuu ya benki hiyo, mkoani Dar es Salaam.
Alidai kuwa katika kipindi hicho, washtakiwa kwa udanganyifu na bila haki waliiibia benki hiyo Sh1,029,454, 383.
Alidai kuwa Mtoro akiwa mtumishi NMB makao makuu, Dar es Salaam, aliingiza maingizo yasiyo sahihi katika akaunti maalumu na kuhamisha Sh579.8 milioni kwenda akaunti binafsi ya Kindamba.
Pia, alidai kuwa Mtoro alihamisha Sh389 milioni kutoka akaunti ya NMB kwenda akaunti ya Cariton Trading Co. Industrial na kwamba pia alihamisha tena Sh60.5 milioni kwenda akaunti ya Jacques Investment huku akijua kuwa fedha hizo ni zao la wizi.
Katika shtaka lingine, Mtoro anadaiwa kutakatisha fedha haramu kwa kubadilisha fedha walizojipatia kwa njia zisizo halali kwa kununua nyumba maeneo ya Mbezi.
Kwa upande wake, Kindamba anadaiwa kutakatisha Sh579,887,395 ambazo zilikuwa zimehamishwa na Mtoro kutoka akaunti ya NMB kwa udanganyifu na kwamba sehemu ya fedha hizo alinunulia nyumba maeneo ya Mabibo.
Mshtakiwa Kikopa kwa upande wake anadaiwa kutakatisha Sh389 zilizohamishwa kutoka akaunti ya NMB na Mtoro kwenda akaunti ya Cariton ambayo yeye alikuwa mtiaji saini pekee.
Pia anadaiwa kutakatisha Sh60 milioni na kwamba sehemu ya fedha hizo ambazo ni Sh449,566,988 alinunulia nyumba maeneo ya Mbezi Mshikamano.
Washtakiwa walikana mashtaka na Hakimu Hellen Liwa anayesikiliza kesi hiyo aliiahirisha hadi Agosti Mosi k watakaposomewa maelezo ya awali

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI