NEC YAWAPIGA MSASA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KUHUSU MABORESHO YA DAFTARI LA KUDUMU WAPIGA KURA KWA KUTUMIA MASHINE ZA KIBALOJIA ZA BIOMETRIC (BVR)
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa akilalamika kuhusu utaratibu usiofaa ulioandaliwa na NEC wa kuionesha na kuielezea mashine yenye teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration (BVR) itakayotumika katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotarajia kuanza Septemba, mwaka huu. Kutoka kulia ni Katibu wa Oganaizesheni wa CCM, Mohammed Seif Khatib, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam juzi, kuhusu mfumo mpya wa maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura baada ya kuhudhuria mkutano viongozi wa vyama vya siasa ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuelezea maandalizi ya maboresho hayo.
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lisu akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam , akiulalamikia mfumo mpya wa kibailojia wa maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wa Biometric Voter Registration (BVR).
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, baada ya kuhudhuria mkutano viongozi wa vyama vya siasa ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuelezea maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Moja ya mashine za kibailojia aina ya Biometric Voter Registration (BVR), zitakazotumika katika uboreshaji wa daftari hilo. Registration (BVR)
Comments