POLISI AMRUBUNI MWANAFUNZI AENDA KULALA NAE NYUMBANI KWAKE HUKU NYUMA NYUMBA ALIYOACHIWA MWANAFUNZI ALINDE YAUNGUA NA MTOTO KUFA

Wananchi wa Mlangali  Ludewa  wakiwa  wamekizingira  kituo cha polisi Mlangali  mara baada ya  kuipeleka maiti ya mtoto aliyeteketea kwa  moto katika  kituo hicho
Wananchi  Mlangali  Ludewa  wakiwa  wamekizingira kituoa  cha polisi cha Mlangali jana
Kitanda ambacho mtoto  huyo alikuwa amelala
Dirisha  likiwa limevunjwa ili  kuutoa mwili wamtoto aliyeungua kwa moto
Wananchi  wakitazama chumba  alichokuwa amelala mtoto  huyo aliyeteketea kwa  moto
 Nyumba  ya askari  iliyodaiwa  kutumika  kufanya mapenzi na mwanafunzi huyo kabla ya mtoto kutetekea kwa  moto
.................................................................................................................
KIONGOZI  wa  mbio  za mwenge  Kitaifa awatuliza wananchi wa Mlangali wilaya ya Ludewa ambao baadhi yao  waliandamana kituo cha polisi kushinikiza kutolewa kwa askari polisi aliyedaiwa kusababisha kifo cha mtoto ili auwawe .
 kiongozi  huyo aliwaomba  wananchi wa Mlangali kutokubali  kujihusisha na vitendo  vya uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na kuepuka  kujichukulia  sheria mkononi  kutokana na  wananchi  zaidi ya 200 jana kuvamia kituo cha polisi Mlangali na kuacha  kushiriki mbio za mwenge kutokana na mmoja kati ya askari kudaiwa kusababisha mauwaji ya mtoto wa miaka 2.
Mbali ya kiongozi  huyo kuwaomba wananchi  kutofanya  vurugu hizo na kutaka  kuacha  vyombo vya usalama kulifanyia kazi bado wananchi hao  waliendelea  kukizunguka kituo  hicho cha polisi hadi majira ya mchana huku mwili  wa  mtoto  huyo ukiwa  umepelekwa kituoni  hapo baada ya  kuungua vibaya kwa  moto.
Wananchi  hao  walifikia  hatua  hiyo ya kuzingira kituo  cha  polisi kutokana na kifo cha mtoto Angela Mtitu kufariki dunia  kwa moto wakati  askari polisi aliyetambuliika kwa jina moja la  kabasa  kudaiwa  kumrubuni mwanafunzi  wa kidato cha tatu katika shule  moja ya  sekondari wilayani Ludewa ambae  ndie  alikuwa akimlea mtoto huyo na kwenda  kufanya nae mapenzi nyumba ya pili ambako ni nyumbani kwa askari  huyo na kupelekea  mtoto huyo kuungua moto.
Hivyo  wananchi hao  wenye hasira kali  walilazimika  kukizingira  kituo  hicho kwa  zaidi ya masaa matano kabla ya askari wa FFU kutoka mkoani Njombe  kufika eneo hilo na kuwatawanya kwa  mabomu ya machozi huku mwili wa mtoto huyo ukiwa ndani ya kituo cha polisi pamoja na askari  huyo na binti huyo mwanafunzi ambao walikuwa  wakishikiliwa na jeshi la polisi.
Kamanda  wa  polisi  wa mkoa wa Njombe hakuweza kupatikana kuzungumzia undani wa  tukio hilo japo baadhi ya askari  waliokuwepo  eneo la tukio  walidai kuwa  tukio hilo lilitokea usiku  wa  kuamkia.

Mtandao huu www.jamvilahabari.com ulifanya mawasiliano na baadhi ya wananchi hao walidai kuwa baba wa mtoto huyo alikamatwa na polisi kwa kesi ambayo ambayo haipo wazi lakini wanadai mzazi huyo kuwekwa kizuizini ni mbinu ya askari huyu ili aendelee kujivinjari na mwanafunzi huyu wa Ulayasi sekondari.

Pia katika vurugu hizo inadaiwa askari wa kutuliza ghasia walitumia mwanya wa vurugu hizo kupora mali katika baadhi ya sehemu za biashara. 

Wananchi hao wamesema walikwenda polisi kuripoti kupotelewa kwa mali zao wanadai mkuu wa kituo anasema hawezi kupokea malalamiko yao kwakuwa jambo hili lipo ngazi za juu, kituhicho kimewafanya wanachi hao washindwa kuelewa wapi ni sehemu sahihi yakupeleka malalamiko yao.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU