Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifuatana
na Mshauri wa Rais Uwekezaji Bw. Abrahman Mwinyi Jumbe (kushoto) akitembelea
shamba la ufugaji wa samaki la kikundi cha Hakiliki Mwambe, Kusini Pemba
jana.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza
na Wananchi wa kikundi cha Ufugaji wa Samaki cha Hakiliki Mwambe, Kusini Pemba
jana. Wapili kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdilahi Jihadi
Hassan.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiteta na
watoto wa Kijiji cha Mwambe mara baada ya kuzungumza na wananchi wa kikundi cha
Ufugaji wa Samaki cha Hakiliki jana, alipofanya ziara katika Mkoa wa Kusini
Pemba.
Wananchi
na waumini wa Dini ya Kiislamu wa vijiji mbali mbali vya Mkoa wa Kusini, Pemba
wakijumuika pamoja katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, kwa wananchi hao
katika viwanja vya Ikulu, Chake Chake Pemba jana.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (wa
nne kulia), akijumuika na viongozi na wananchi mbali mbali wa Mkoa wa Kusini
Pemba katika futari aliyowaandalia jana katika viwanja vya Ikulu, Chake
Chake.
Baadhi
ya akinamama wa Mkoa wa Kusini Pemba wakijumuika kwa pamoja katika futari
waliyoandaliwa na mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mwanamwema Shein (hayupo
pichani) katika ukumbi wa Ikuu ya Chake chake jana.
Mke wa
Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Chake chake
Pemba Mwanajuma Majid katika futari aliyowaandalia wananchi wa Vijiji mbali
mbali vya Mkoa wa Kusini Pemba hafla hiyo, ilifanyika jana katika ukumbi wa
Ikulu ya Chake Chake.
Comments