RASMI: MATHIEU DEBUCHY AMRITHI BACARY SAGNA ASERNAL KWA DAU LA PAUNDI MILIONI 10


 

 


Announcement: Arsenal made the transfer public on their twitter with a picture of the new signing
Tangazo rasmi: Arsenal walitangaza hadharani usajili huo kupitia mtandao wake wa Twita ambapo waliweka picha na ujumbe.

Imechapishwa Julai 18, 2014, saa 1:45 asubuhi

KLABU ya Arsenal imemsajili beki wa kulia wa Ufaransa Mathieu Debuchy kutokea  klabu ya Newcastle.
Debuchy, mwenye miaka 28, amesajiliwa kwa nia ya kuziba pengo la beki wa kulia, Mfaransa mwenzake, Bacary Sagna aliyetimka Emirates na kujiunga na mabingwa wa ligi kuu, Manchester City majira haya ya kiangazi mwaka huu.
Asernal alitweet picha ya Debuchy ikisindikizwa na ujumbe uliosomeka #Karibu Debuchy.
Pedigree: Debuchy played four of France's five World Cup matches as Les Bleus impressed in Brazil
Jembe jipya: Debuchy aliichezea Ufaransa mechi nne kati ya tano za kombe la dunia nchini Brazil na alionesha kiwango cha juu. 
Welcome: Arsenal's official Instragram posted a picture of the Frenchman's new shirt
Karibu: Pia Arsenal iliposti picha ya jezi ya mfaransa huyo kwenye mtandao wake rasmi wa  Instragram.

Debuchy alijivunia usajili huo na akasisitiza kuwa umuhimu wa ligi ya mabingwa ndio kichocheo cha yeye kujiunga na Asernal.
"Najivunia kujiunga na klabu kubwa kama hii na kuvaa rangi zake, ni moja ya klabu kubwa zaidi duniani," beki huyo wa kulia aliuambia mtandao wa Asernal.com.
"Naangalia mbele nikiwa na Aserne Wenger na kuisaidia timu kuendeleza mafanikio ya msimu uliopita ya kutwaa kombe la FA".
"Kucheza tena ligi ya mabingwa ni fuaraha kubwa kwangu na nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kuisaidia Asernal kushindania kombe"
Replacement: Debuchy arrives at Arsenal to replace Bacary Sagna who he has displaced in the France side
 Debuchy amewasili  Arsenal kurithi mikoba ya Bacary Sagna ambaye hakuonesha kiwango kikubwa katika fainali za kombe la dunia akiwa na Ufaransa.
Striking a pose: Debuchy said he was excited to be playing Champions League football again
Pozi bab kubwa!: Debuchy alisema amefurahi kucheza ligi ya mabingwa tena. 
Looking up: The new signing will be Arsenal's first choice right-back after Sagna joined Manchester City
Ametokelezea: Nyota huyu atakuwa chaguo la kwanza katika nafasi ya beki wa kulia baada ya kuondoka kwa Sagna aliyejiunga na Manchester City
Welcome: Arsene Wenger highlighted Debuchy's top-level experience as a key reason for signing the Frenchman
Karibu: Arsene Wenger aliweka wazi kuwa uzoezi mkubwa wa Debuchy ndio sababu ya msingi ya kumleta kikosini beki huyo Mfaransa

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI