Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akipokea galoni ya
mafuta ya kula kutoka kwa Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada (kushoto)
ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya chakula cha msaada kwa ajili ya Wakimbizi
kilichotolewa na Serikali ya Japan. Kulia ni Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi
wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Richard Regan akipokea msaada huo
kutoka kwa Waziri Chikawe ambao una thamani ya Dola za Marekani 1.4
sawa na zaidi ya Shilingi 2.3 bilioni katika tukio la makabidhiano lililofanyika
jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupokea msaada wa
chakula kwa ajili ya Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, mkoani Kigoma
chenye thamani ya Dola ya Marekani 1.4 sawa na zaidi ya Shilingi 2.3
Bilioni, ambazo zimetolewa na Serikali ya Japan. Kushoto ni Balozi wa
Japan nchini, Masaki Okada na Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Shirika
la Chakula Duniani (WFP), Richard Regan. Waziri Chikawe alipokea msaada
huo na kumkabidhi Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa WFP, Regan, Bandari
ya Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe
(katikati) akimshukuru Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada (kushoto)
kwa msaada wa chakula wenye thamani ya Dola za Marekani 1.4
milioni ambao ni sawa na Shilingi 2.3 Bilioni ambao Serikali yake imetoa
kwa ajili ya Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, mkoani Kigoma. Kulia ni
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Richard Regan
ambaye alikabidhiwa msaada huo baada ya Waziri Chikawe kuupokea katika
sherehe fupi ya makabidhiano iliyofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO
YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Comments