VIJANA WAASWA KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO

                

IMG_4958Afisa Kata wa Kata ya Mchinga, Bi. Sharifa Mkwango, akisisitiza jambo kuhusu vijana kujiunga katika vikundi vya uzalizashaji mali.
IMG_4923Vijana  wa  Kata ya Mchinga, Lindi Vijijini  wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi  (hayupo pichani) wakati akiwaelekeza namna ya kuunda vikundi na kupata mikopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana mwishoni mwa wiki.
IMG_4936
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi akisisitiza jambo wakati akiwahamasisha vijana wa Mchinga kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali ili kuunda SACCOS ya vijana. Kulia ni Afisa Tarafa ya Mchinga, Bi.Hadija Mringwa.
 
(Picha zote na Concilia Niyibitanga
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo)
Na Concilia Niyibitanga
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
 Serikali imewataka vijana Mchinga kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kujiinua kiuchimi na kuleta maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw. James Kajugusi alipokuwa anaongea na Vijana wa Halmashauri ya Lindi Vijijini Kata ya Mchinga jana  kuhusu masuala ya maendeleo ya Vijana.
Bw. Kajugusi amewaeleza vijana umuhimu wa kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali  ili kuunganisha nguvu za kimtaji na kufikiri kwa pamoja namna ya kuboresha maisha yao ya kila siku.
Vijana wanapokuwa katika vikundi ni rahisi sana kutambulika nani yuko wapi anafanya nini na anahitaji nini hivyo kuirahisishia Serikali kuwasadia. Amesema Bw. Kajugusi.
Amesema kuwa kijana wa sasa anatakiwa kujitambua na kujua kuwa yeye ndiyo tegemeo la taifa hivyo kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo yeye mwenyewe na taifa kwa ujumla.
Changamoto kubwa ya vijana ni kutojitambua hivyo kufikiri kwamba wanahitaji mitaji kwanza wakati bado hawana hata wazo la kuwekeza na mtaji huo. Amesema Bw. Kajugusi.
Amesema kuwa ni muhimu vijana hao wakajiunga katika vikundi vya uzalishaji mali ili waweze kuunda SACCOS yao kwa ajili ya kupata fedha ya mkopo kutoka katika Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili kukuza mtaji na kuzalisha mali kwa ajili ya maendeleo endelevu.
Bw. Kajugusi amewaeleza kuwa kupitia SACCOS ya vijana wataweza kupatiwa mikopo yenye riba nafuu ya asilimia 10 ya mkopo ambapo asilimia 5 ya riba hiyo inabaki kwenye SACCOS husika, asilimia 2 inabaki Halmashauri na asilimia 3 inarudi mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili kuutunisha na kuwawezesha vijana wengine kukopa.  
Aidha, amewataka vijana kujali afya zao hususan kuepuka matumizi ya dawa za kulevya kwani yanaharibu akili na viungo vya mwili hivyo kuathiri kiwango cha kufikiri na kuathiri utendaji kazi na uzalishaji wa kijana.
Halikadhalika, amewataka kujikinga na magonjwa ya zinaa na mimba za utotoni ili kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya jamii.
Naye Afisa Tarafa ya Mchinga, Bi. Hadija Mringwa aliwataka vijana wa Kata hiyo kuhakikisha kuwa wanakamilisha zoezi la kujiunga katika vikundi na kuanzisha SACCOS mapema iwezekanavyo ili waweze kufaidi fursa ya mkopo kutoka katika Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.