WAKUU WA SHULE ZA SERIKALI ZILIZOFANYA VIBAYA KATIKA MATOKEO YA FORM SIX WAPEWA MWEZI MMOJA KUJIELEZA.....MIONGONI MWA SHULE HIZO NI TAMBAZA NA IYUNGA

Wakuu wa shule za serikali zilizofanya vibaya kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu  pamoja na Maofisa elimu wa Mikoa wamepewa muda wa mwezi mmoja ili kubaini chanzo cha  shule zao kuwa na ufaulu hafifu.
 Baada ya kubaini chanzo hicho cha ufaulu hafifu wanatakiwa kutoa taarifa kwa katibu mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa-TAMISEMI.
 Miongoni mwa shule ambazo wakuu wake wametakiwa kujieleza ni pamoja na shule ya Tambaza iliyopo jijini Dar es salaam na shule ya Iyunga ya Mkoani Mbeya, ambapo muda huo wa mwezi mmoja umeanza  leo.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam,  katibu Mkuu Tamisemi Jumanne Sagini amesema, kushuka kwa ufaulu kwa shule hizo kumewashtua  watu wengi, kwani shule hizo zimejengewa uwezo mzuri wa vifaa pamoja na miundombinu.
 
Hata hivyo Sagini amesema, idadi ya wanafunzi 22,685 waliofaulu masomo ya sayansi kwa mwaka  huu wa 2014  ni kubwa kwa  zaidi ya wanafunzi 3,939 ikilinganishwa na wanafunzi 18,746  waliofaulu masomo hayo mwaka jana.
 
Amesema kuwa ufaulu huo umeipa changamoto Serikali na imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi ambae amefaulu na kupata alama stahiki  katika masomo aliyoyachagua anapata shule.
 
Aidha amewataka wazazi wa wanafunzi waliokuwa wamepangiwa kusoma masomo ya sanaa ilihali ufaulu wao ni katika masomo ya sayansi, kutokuwa na wasiwasi kwani serikali imebaini changamoto hiyo na kuifanyia kazi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA