YAYA TOURE HANG`OI `GUU` LAKE, ATAKA KUZEEKEA MAN CITY


 
 

KIUNGO wa mabingwa wa England, Manchester City, Yaya Toure amesema anataka kubakia klabuni hapo kwa muda mrefu kadiri itakavyowezekana.
Nyota huyo mwenye miaka 31 mapema mwaka huu aliripotiwa kutimka Etihad baada ya wakala wake, Dimitri Seluk kusema kuwa Toure alijisikia kutothaminiwa na klabu baada ya kutotumiwa salamu za siku ya kuzaliwa mwezi mei.
Toure mwenye alieleza kuwa anavutiwa kujiunga na matajiri wa Ufaransa, Paris Saint-Germain.
Siku za nyuma Toure alisema kwamba, mashabiki wasisikilize maneno ambayo hayajatoka mdomoni mwake, lakini kila asemacho Dimitri ni sahihi kwasababu anazungumza kwa niaba yake, ingawa kwasasa anasisitiza kuwa wakati wote amekuwa kimya kuhusu furaha yake na hatima yake ya baadaye.
Muivory coast huyo aliiambia tovuti ya klabu kuwa ana nia ya kuendelea kubakia Man City, na aliongeza kuwa ameweza kukabiliana vizuri na tetesi za yeye kuondoka Etihad.
Toure alieleza: “Halikuwa jambo la kuondoka klabuni, ni ngumu sana kwasababu mazingira yangu ni magumu. Tunapotakiwa kufanya kitu fulani, tulitakiwa kutoa maelezo. Kwangu mimi ni kawaida…mara zote nilikuwa kimya”.
“Na mwisho wa siku ni maamuzi yangu. Kama unaseme kwamba, nitasema kwamba. Kama hupendi hilo, nitasema tena hilo na kama unapenda hilo, nitasema, kwangu mimi ni jambo sahihi, na nitakaa Man City kwa muda mrefu kadiri iwezekanavyo”.
Toure alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Manuel Pellegrini kilichotwaa ubingwa akifunga mabao 20 katika michezo 35 aliyocheza msimu uliopita, lakini amesisitiza kuwa City lazima ijipange kuelekea msimu wa 2014/2015 kwasababu ya vipaji vinavyoendelea kufurika katika klabu za ligi kuu.
“Kwasasa nina furaha ya kujiunga na timu na kocha kwasababu ni kocha wa ajabu,” Alisifu. “Kila mtu ana furaha. Mwaka uliopita ulikuwa msimu mzuri”.
“Mwaka huu utawakuwa wa kushangaza kwasababu timu zote kubwa zinasajili wachezaji wazuri. Kwa upande wangu, jambo la kwanza ni kurudi kwa nguvu tena”.
Toure alikiri kuwa miezi michache iliyopita, yeye na familia yake walikuwa katika hali ya huzuni kufuatia kufariki kwa kaka yake, Ibrahim baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.

“Najisikia vizuri,” alisema kiungo huyo. “Ni vizuri nimeanza mazoezi tena. Kwa bahati mbaya wakati wa mapumziko ulikuwa mgumu kwa familia yangu”.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.