ZIARA YA RAIS KUFUNGUA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU MKUZO, SONGEA

            


Rais Jakaya Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh. Saidi Mwambungu kulia , Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. David Shambwe wakikata utepe kwa pamoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.

 Rais Dr. Jakaya Kikwete akipata taarifa ya mradi huo wa nyumba za gharama nafuu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw  David Shambwe

  Rais Dr. Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo 

 Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwasili  katika eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba  (NHC) na kupokelewa na Ndg. David Shambwe Kaimu Mkurungenzi Mkuu NHC na Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wakati alipokagua mradi huo uliopo katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma  akiwa katika ziara yake ya kikazi leo, Rais Dr. Jakaya Kikwete anaendelea na ziara mkoani  humo leo. (PICHA ZOTE KWA HISANI YA KITENGO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII CHA NHC)

 Rais jakaya Kikwete akipata maelezo ya kuhusu Mashine za kufyatulia matofali  ambazo zimegawiwa kwa kila wilaya za mkoa wa  Ruvuma

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akizungumza katika hafla hiyo mchana huu

 Akiwasalimia wananchi waliofika kushuhudia


Vikundi vya nguma na burudani ikiburudisha katika tukio hilo mchana wa leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, alipofungua leo hii nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC katika eneo la Mkuzo, Mkoani Ruvuma.
Kwa ujumla Mh. Rais alisema yafuatayo:-
      Amerejea kauli yake aliyoitoa Kasera , Mkinga Tanga kwa kulipongeza Shirika kwa kazi nzuri linayofanya hususan ya uamuzi wake wa  kizalendo wa kujenga nyumba za watu wa kipato cha kati na chini katika Halmashauri za Miji na Wilaya hapa nchini.
      Alizitaka Halmashauri za Miji na Wilaya kulipatia Shirika pamoja na mashirika na mifuko mingine ya jamii kama NSSF, PPF, LAPF, GEPF na mengineyo ardhi yenye masharti nafuu ili kuwezesha ujenzi wa nyumba na hatimaye kuweza kuipanga miji ipasavyo.
      Aliziagiza Halmashauri hasa ya Songea kutumia fursa za mikopo kutoka benki washirika na NHC kuweza kununua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa badala ya kuendelea na mtindo wa kutaka kupanga nyumba hizo..
     Alilipongeza Shirika kwa kuwezesha vijana mashine za kufyatulia matofali jambo ambalo litatoa ajira kwa vijana. Alifurahishwa na mpango huo na kuzitaka Halmashauri nchini kuusaidia mpango huo ili uwe endelevu na wenye manufaa kwa vijana.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA