AZAM FC YATUPWA NJE KAGAME CUP YALAZWA PENATI 4-3 NA EL MARREIKH YA SUDAN

Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa AfrikaMashariki na Kati, Kombe la Kagame,  Azam FC ya Chamanzi jijini Dar es Salaam imetupwa nje ya michuano hiyo mikubwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kucharazwa mikwaju 4-3 dhidi ya El Marreikh ya Sudani katika mchezo wa pili wa robo fainali.Wachezaji ambao walielezwa awali kuwa wanasumbuliwa na vyama za paja lakini wakashuka katika dimba la Nyamirambo mjini Kigali Rwanda ndio walioigharimu Azam FC licha ya mlinda mlango  Mwadin Ally kufanya kazi nzuri ya kupangua penati ya wapinzani wao. 

Wachezaji walioipa tiketi ya kurejea nyumbani Azam FC kujiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga SC ni beki Shomary Kapombe na mshambuliajiLionel Saint- Preux kutoka Haiti.
Aidha kocha wa mabingwa hao wapya wa soka la Tanzania, Mcameroon JosephMarious Omog ameonekana amekuwa akiandaa Azam FC kitaalamu mnokuelekea mchezo huo, ambapo mbali na mambo mengine aliwaelekeza mifumona aina tofauti ya uchezajiikiwa ni pamoja na kutumia mipira mirefu na mifupi.
Omong aliwaandaa wachezaji wake pia kwa kupiga penaltilakini hakuna kilichofua dafu kutokana na upigaji wa kimakosa uliofanywa na Kapombe aliyepaisha penati yake juu na gonga mwamba na Preux aliyepiga mpira mwepesi na kumwezesha mlinda mlango wa Merreikh kuificha bila shaka.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.