BAADA YA KIPIGO CHA SERENGETI BOYS, MALINZI AKIRI UBOVU WA MAANDALIZI NA KUKOSEKANA KWA MFUMO SAHIHI WA SOKA LA VIJANA

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
BAADA ya timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys kutolewa katika michezo ya kuwania kufuzu fainali za Afrika za vijana na Afrika kusini kwa wastani wa mabao 4-0, Rais wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Jamal Emil Malinzi amekiri kuwa bado timu haijaandaliwa vizuri.
Rais Malinzi amesema tatizo la timu ni maandalizi yasiyoridhisha yanayochangiwa na kukosa mfumo sahihi na mpango mzuri wa soka la vijana.
“Tatizo letu ni lile lile, kwenye maandalizi, lakini tunapozungumzia maandalizi tunazungumzia uwezo wa kiuchumi, kwamba timu yetu inaandaliwaje,” Alisema Malinzi.
“Tunaweza kusema timu imejitahidi, Lakini kiukweli hii ndio mechi yao ya pili ya kimataifa, mechi yao ya kwanza walicheza na Afrika kusini nyumbani,
“ Kwahiyo lazima sisi tukae kama nchi,  kama shirikisho ili tuweze kuangalia programu zetu za soka la vijana ili watoto kama hawa kabla hawajaingia katika mechi kama hizi wawe wameshakaa kama timu kuanzia umri wa 12, 13, 14 na 15 , yaani wakae miaka minne kwenye timu ya taifa,” Aliongeza Malinzi.
Aidha, Rais Malinzi alisema shirikisho hilo limejipanga upya ili kuhakikisha nchi inakuwa na mfumo sahihi wa soka la vijana.

“Kipo ambacho kinafanyika, tunaandaa mpango wa kitaifa wa maendeleo ya soka la vijana na tutazindua mwezi wa 10 mwaka huu, siku ambayo TFF itatimiza miaka 10 ya kujiunga na FIFA na tutaeleza haya tunayoyasema ili kama nchi tuwe na mpango endelevu wa soka la vijana,”

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI